Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 7 - Mungu Anayo kazi Kwako Kufanya

  K.AZI ya Mungu duniani humu kamwe haiwezi kumalizika mpaka wanaume na wanawake walio washiriki wa kanisa letu wapate moyo tena kwa kazi na kushirikiana kwa umoja katika jitihadi zao na wachungaji na waongozi wa kanisa. 19T 117;KN 67.1

  Maneno haya “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.” (Marko 16:15) yamesemwa kwa kila mmoja wa wafuasi wa Kristo. Wote waliotoa maisha yao kwa Kristo wameamriwa kufanya kazi kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wenzao. Shauku ile ile aliyoona moyoni kwa ajili ya wokovu wa waliopotea yapasa kudhihirishwa ndani ya wafuasi wake. Wote hawawezi kusnika kazi ile ile, lakini kuna nafasi na kazi kwa wote. Wote waliojaliwa mibaraka ya Mungu wamepaswa kuitikia kwa kufanya kazi hasa; kila kipawa hakina budi kutumiwa kwa kueneza ufalme wa Mungu. 28T 16;KN 67.2

  Kuhubiri ni sehemu ndogo ya kazi ipasayo kutendwa kwa ajili ya wokovu wa roho za watu. Roho wa Mungu huwasadikisha wenye dhambi Neno la kweli, naye huwaweka katika mikono ya kanisa. Wachungaji huenda wakafanya sehemu yao, lakini, kamwe hawawezi kufanya kazi ambayo kanisa lingefanya. Mungu anataka kanisa lake kuwalea wale ambao ni wachanga katika imani na maisha, kuwaendea, si kusudi kupiga porojo nao, bali kusali, kuzungumza nao maneno ambayo yatawaimarisha katika imani. 34T 69;KN 67.3

  Mungu ameliita kanisa lake siku hizi, kama alivyowaita Waisraeli wa zamani za kale, kusimama kama nuru duniani. Kwa nguvu nyingi za neno la Mungu, ujumbe wa malaika wa kwanza , wa pili na wa tatu, amewatenga kutoka kwa madhehebu nyingi na kutoka kwa walimwengu kuwaleta karibu naye mwenyewe. Amewafanya watunzaji wa sheria yake na amewakabidhi maneno makuu ya unabii wa wakati huu. Kama maneno matakatifu aliyosema Mungu yalivyokabidhiwa kwa Waisraeli wa zamani zile za kale, haya ni amana takatifu ipasayo kutolewa kwa ulimwengu.KN 67.4

  Malaika watatu wa Ufunuo 14 ni mfano wa watu ambao huipokea nuru ya ujumbe wa Mungu na kwenda kama mawakili waKe kutangaza onyo hili pande zote duniani. Kristo anawaambia wafuasi wake: “Ninyi ni nuru ya ulimwengu”( Mathayo 5:14). Kwa kila mmoja amkubaliye Yesu, msalaba wa Kalwari unasema: “Tazama thamani ya roho ya mtu. ‘Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe,” (Marko 16:15). Pasiruhusiwe kitu cho chote kuzuia kazi hii. Ni kazi ya maana kabisa kwa wakati huu, ni ya kudumu hata milele. Upendo ambao Yesu ameuonyesha kwa ajili ya roho za watu kwa dhabihu aliyoitoa kwa ajili ya wokovu wao, utawabidiisha wafuasi wake wote. 45T455, 456;KN 67.5

  Kristo hukubali hasha kwa furaha! Kila njia ya binadamu ambayo imetolewa kwake humwingiza mwanadamu kwenye umoja na Mungu, ili Mungu apate kuwapasha walimwengu habari za maajabu ya upendo wa Yesu Kristo Kufanyika mtu halisi. Ongea juu yake, Omoa juu yake, na zidi kusonga mbele mpaka ng’ambo ya pili. 59T 30;KN 68.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents