Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mafundisho Juu ya Kubadili Chakula

  Ni kosa kudhani kwamba nguvu za musuli hutegemea juu ya kutumia chakula cha nyama. Mwili waweza kupatiwa mahitaji yake vizuri zaidi, na kuwa na afya bora bila kutumia nyama. Nafaka, pamoja na matunda, njugu, na mboga za majani, vina lishe yote ya chakula inayolazimu kuifanya damu iwe nzuri. Vitu hivyo havipatikani vizuri wala kamili kwa chakula cha nyama. Kama kutumia nyama kungekuwa jambo bora kwa afya na nguvu, nyama ingalikuwa miongoni mwa chakula alichoamriwa mwanadamu mwanzoni.KN 261.4

  Nyama ikiachwa kutumiwa, mara nyingi mtu hujiona kuwa ana udhaifu, na asiye na nguvu. Wengi husisitiza neno hili kama jambo linalothibitisha kuwa nyama ni kitu bora; lakini ni kwa sababu vyakula vya watu hao ni vyenye kusisimua nguvu mwilini, kwa kuwa huitia damu homa na kusisimua neva, ndiyo maana wanatamani sana kuvipata. Wengine wataona shida kuacha kula nyama sawa na ilivyo kwa mlevi kuacha kiasi kidogo cha ulevi wake, lakini itawafaidia kubadili.KN 261.5

  Chakula cha nyama kikikataliwa, yafaa badala yake pawepo nafaka, njugu, mboga za majani, na matunda; vitu ambavyo vitatia mwili afya na vyenye utamu. Hilo hulazimu hasa kwa wale ambao ni wadhaifu, au wenye kutumikishwa kazini daima. 16MH 316;KN 262.1

  Hasa mahali ambapo nyama haifanywi chakula kikuu ni bora kupika vitu muhimu. Kitu fulani hakina budi kutayarishwa kuwa badala ya nyama, na vitu hivyo vilivyo badala ya nyama havina budi kutayarishwa vizuri, kusuai nyama isitamamke tena. 17CG 384;KN 262.2

  Naiua jamaa ambao wamekiacha chakula cha nyama na kutumia chakula cha kimaskini. Chakula chao hupikwa ovyo sana hata tumbo hukichukia kabisa; watu kama hao wameniambia kuwa kutokula nyama si jambo wanalopatana nalo, kwamba wamekuwa wakipungukiwa na nguvu za mwili. Yafaa chakula kitayarishwe bila kukolezwa kwa viungo, lakini kiwe na ladha. 182T 63;KN 262.3

  Ni kwa faida yao wenyewe kwamba Mungu hulionya kanisa la masalio kuacha kutumia nyama, majani ya chai, na kahawa, na vyakula vingine vyenye madhara. Kuna vitu vingine vingi tuwezavyo kuponea ambavyo ni vya kufaa.KN 262.4

  Miongoni mwa wale wenye kungojea kuja kwa Bwana, wataachilia mbali kula nyama hatimaye; nyama itakoma kuwa sehemu ya chakula chao. Yatupasa kukumbuka mwisho huo daima, na kujitahidi kufanya kazi kwa uaminifu kuukaribia. 19CD 380, 381;KN 262.5

  Nguvu za akilini, moyoni, na mwilini hupunguzwa na mazoea ya kutumia nyama. Kula nyama huharibu mwili, nuduwaza akili, na kupunguza nguvu za fahamu za moyoni. Twawaambieni, ndugu na dada wapendwa, njia ya salama kabisa kwenu ni kutotumia nyama. 202T 64.KN 262.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents