Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Fikira za Mungu kwa Kila Mmoja wa Watoto Wake

    Maandiko Matakatifu huonyesha dhahiri uhusiano baina ya Mungu na Kristo, nao hudhihirisha wazi nafsi ya kila mmoja. Mungu ni Baba wa Kristo; Kristo ni Mwana wa Mungu. Kristo amepewa cheo cha juu. Amefanywa sawa na Baba Mashauri yote ya Mungu hufunuliwa kwa Mwanawe. Umoja huu huelezwa pia katika sura ya kumi na saba ya Yohana, katika sala ya Kristo kwa ajili ya wanafunzi wake:KN 89.1

    “Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenltuma ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.” (Yohana 17:20-23).KN 89.2

    Maneno ya ajabu! Umoja uliopo baina ya Kristo na wanafunzi wake hauharibu nafsi ya ye yote kati yao wawili. Wanalo kusudi moja, nia moja, tabia moja, lakini si nafsi moja. Hivyo ndivyo Mungu na Kristo walivyo mmoja.KN 89.3

    Mbingu na nchi zimo chini ya amri ya Mungu wetu, naye ajua kile hasa tunachohitaji. Twaweza kuona kidogo tu njia iliyo mbele yetu; “lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.” (Waebrania4:13). Juu ya uharibifu wa duniam aketi hali amevikwa taji; mambo yote ni wazi kwa uchunguzi wake wa kimungu; na kutoka katika ukuu na utulivu wake wa milele huamuru kile ambacho amri yake Mungu yaona ni bora.KN 89.4

    Hata shomoro mmoja haanguki chini pasipo Baba kujua. Chuki ya Shetani juu ya Mungu humwongoza kufurahia kuviangamiza viumbe visivyoweza kusema. Ulinzi wa Mungu tu ndio unaowalinda ndege na kuwahifadhi ili wapate kutupendeza kwa nyimbo zao za furaha. Lakini hawasahau hata shomoro. “Msiogope basi; bora ninyi kuliko mashomoro wengi.” (Mathayo 10:32). 28T263-273KN 89.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents