Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Njozi ya Vita Kuu Baina ya Kristo na Shetani

    Nyumba ndogo ya shule katika kijiji kimoja upande wa mashariki ya Amerika ilikuwa imejaa wanaume na wanawake siku ile ya Jumapili alasiri katikati ya mwezi wa Machi, 1858, walipokuwa wamekusanyika kwa ibada. Mchungaji James White aliongoza mazishi ya kijana wa kiume, akihubiri mahubiri ya mazishi. Alipomaliza kusema, Ellen G. White aliguswa moyoni kusema maneno machache kwa wale waliokuwa wakiomboleza. Akasimama na kusema kwa dakika moja au mbili na kisha akanyamaza. Watu wakatazama juu ili kuyasikia maneno mengine kutoka midomoni mwake. Wakashangazwa kidogo na msemo wa ghafula wa maneno haya “Atukuzwe Mungu!” “Atukuzwe Mungu!” uliorudiwa mara tatu kwa mkazo zaidi. Ellen G White alikuwa katika njozi.KN 10.1

    Mchungaji White akawaambia watu juu ya njozi alizopewa Ellen G White. Akaeleza kuwa alianza kupewa njozi akiwa kijana mwenye umri wa miaka kumi na saba. Akawaambia kuwa ingawa macho yake yalikuwa yamefumbuka, na ilielekea kana kwamba alikuwa akitazama kitu fulani mbali, alikuwa hana habari za lo lote la mahali alipo na hakujua cho chote kilichokuwa kikitendeka karibu naye. Akataja Hesbu 24:4 na 16 tusomapo habari za mtu “asikiaye maneno ya Mungu, yeye aonaye maono ya Mwenyezi, akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho.”KN 10.2

    Akawaeleza watu kuwa hapumui awapo katika njozi na akageukia Daniel 10:17 na kusoma nali ya Daniel alipokuwa katika njozi. Akasema, “Kwangu mimi, mara hazikusalia nguvu ndani yangu, wala pumzi haikusalia ndani yangu.” Ndipo Mchungaji White akawaomba, waliopenda, waende wampime Ellen G White akiwa katika njozi. Daima alitoa uhuru wa kumpima namna hii, na alipendezwa kama aliweza kupatikana daktari kumpima akiwa katika njozi.KN 10.3

    Kadiri watu walivyosongamana, waliweza kuona kuwa Ellen White hakuwa akipumua, lakini moyo wake uliendelea kupiga kama kawaida na rangi ya mashavu ya uso wake ilikuwa ya kawaida, Kioo kiliposogezwa karibu na pua na mdomo wake, hakuna ukungu uliokusanyika juu ya kioo. Kisha wakaleta mshumaa na kuuwasha na kuushikilia karibu na pua na mdomo wake. Lakini, mwali wa moto ulisimama wima, bila kuyumbayumba. Watu wakajua kuwa alikuwa hapumui. Alikwenda huko na huko chumbani, na kujongeza mikono yake taratibu akisema kwa kasi mambo yaiiyokuwa yakifunuliwa kwake. Kama Daniel, kwanza alipotewa na nguvu zake za asili, kisha akatiwa nguvu zisiso za kawaida. (Tazama Danieli 10:7, 18, 19).KN 10.4

    Kwa muda wa saa mbili Ellen White alikuwa katika njozi. Muda wa saa mbili hakupumua hata kidogo. Kisha kadiri njozi ilivyokuwa inakwisha, akavuta pumzi sana, akanyamaza kwa muda wa dakika moja hivi ndipo akapumua tena, mara akaanza akapumua kwa kawaida. Mara hiyo aliweza kuyajua mazingira yake, na kufahamu mambo yaliyokuwa yakitendeka karibu naye.KN 11.1

    Mtu mmoja ambaye alimwona mara nyingi Ellen White akiwa katika njozi, Bibi Marths Amadon, alitoa maelezo yafuatayo: “Akiwa katika njozi macho yake yalifumbuka. Hakupumua, lakini mabega, mikono, na viganja vya mikono vilisogea taratibu, vikionyesha mambo aliyokuwa akiyaona. Hakuna mtu aliyeweza kuisogeza mikono yake. Mara nyingi alitamka maneno ambayo yaliwaonyesha wale waliokuwa karibu naye hali ya maono aliyokuwa nayo, ama ya mbinguni ama ya dumani.KN 11.2

    “Neno lake la kwanza katika njozi lilikuwa ‘utukufu’ lililosikika kwanza kwa nguvu, na kisha kufifia na kuelekea kana kwamba yuko mbali sana. Hili mara zingine lilirudiwa KN 11.3

    “Wale waliokuwako wakati wa njozi hawakuwa na wasiwasi, wala hapakuwako na jambo lo lote la kuogofya. Lilikuwa jambo la taratibu, na tulivu KN 11.4

    “Njozi ilipokwisha, na kupotewa na nuru ya mbinguni, akirudia dunia hii tena, alisema, alipoanza kupumua kama kawaida “GIZA’. Kisha alilegea na kukosa nguvu.”KN 11.5

    Lakini yatupasa kurejea kwenye ile hadithi yetu ya njozi ya saa mbili shule. Kwa habari ya njozi hii Ellen White baadaye aliandika:KN 11.6

    “Mambo mengi ambayo niliyaona zamani zaidi ya miaka kumi iliyopita juu ya vita ya zama zote baina ya Kristo na Shetani, yalirudiwa, nami naliagizwa kuyaandika.”KN 11.7

    Katika njozi anjiona kuwa alikuwa akiyaona kwa macho mambo hayo kadiri yalivyokuwa yakidhihirika mbele yake. Kwanza ilielekea kana kwamba alikuwa mbinguni naye akashuhudia kwa macho dhambi na kuanguka kwa Nyota ya alfajiri (Lucifer). Kisha alishuhudia uumbaji wa ulimwengu huu na kuwaona wazazi wetu wa kwanza katika makao yao ya Edeni. Akawaona wakishindwa na majaribu ya joka nao wakafukuzwa kutoka makaoni mwao Bustanini. Kwa naraka mfululizo wa historia ya Biblia ukapitishwa mbele yake. Akayaona mambo yaliyowapata watakatifu wa zamani na manabii wa Israeli. Kisha akaona kwa macho maisha, na kufa kwa Kristo Mwokozi wetu, na kupaa kwake mbinguni mahali ambapo tokea hapo amehudumu kama Kuhani wetu Mkuu. Baada ya haya akawaona wanafunzi wa Yesu wakitoka kwenda kueneza ujumbe wa Injili hata miisho ya dunia. Upesi sana jambo hili lilifu- atiwa na uasi na miaka ya giza! Kisha akaona katika njozi Matengenezo (Reformation) ya kanisa, wanaume na wanawake wakiwa katika hatari ya kupoteza maisha yao kwa kusimama na kuitetea kweli. Alionyeshwa mambo ya hukumu ambayo ilianza mbinguni mwaka 1844, na kuendelea mpaka siku zetu, kisha alipelekwa katika mambo ya wakati ujao akaona kuja kwa Kristo katika mawingu ya mbinguni. Aliona mambo ya muda wa miaka elfu na nchi mpya.KN 11.8

    Akiwa na maono haya dhahiri mbele yake, Ellen White alipokwisha kurejea nyumbani kwake alianza kuandika mambo aliyoyaona na kuyasikia katika njozi. Baada ya miezi sita kitabu kidogo cha kurasa 219 kikatoka katika mitambo ya kuchapisha vitabu chenye jina la The Great controversy Between Christ and His Angels and Satan and His Angels, yaani vita Kuu baina ya Kristo na Malaika zake na Shetani na Malaika Zake.KN 12.1

    Kitabu hiki kidogo kilipokelewa kwa moyo mkuu, maana kilieleza dhahiri mambo yaliyokuwa mbele ya Kanisa na kufunua mipango ya Shetani na namna atakavyofanya akijaribu kulipotosha Kanisa na ulimwengu katika vita vya mwisho vya dunia Waadventista walishukuru mno kwamba Mungu alikuwa akisema nao siku hizi za mwisho kwa njia ya Roho ya Unabii, kama alivyoahidi kufanya.KN 12.2

    Habari za Vita Kuu, ambazo zimesimuliwa kwa kifupi sana katika kitabu kidogo cha Spiritual Gifts, yaani, Karama za Kiroho, baadaye zilichapishwa tena katika nusu ya mwisho ya Early Writings..KN 12.3

    Lakini kadiri kanisa lilivyozidi kukua na siku zikapita, Bwana kwa njozi nyingi za baadaye alifunua kisa cha Vita Kuu kwa maneno mengi zaidi, na Ellen White akayaandika tena, kati ya mwaka 1870 na 1884, katika vitabu vinne vilivyoitwa The Spirit of Prophecy yaani Roho ya unabii. Kitabu cha TheStory of Redemption hutoa sehemu za maana zaidi za kisa cha Vita Kuu ambazo zimetwaliwa kutoka katika vitabu hivi. Kitabu hiki ambacho kimechapishwa katika lugha nyingi huwaletea watu mambo vale yaliyoonyeshwa katika njozi hizi za Vita Kuu. Pia Ellen White katika vitabu vitano vya baadaye vya jamii ile ya “Conflict of the Ages Series” -Partriarchs naa Prophets, Prophets and Kings, The Desire of Ages, Acts of the Apostles, na The Great Controversy, - alisimulia habari zote kabisa za Vita Kuu.KN 12.4

    Vitabu hivi ambavyo hulingana sawa sawa na maneno ya Biblia toka uumbaji hadi wakati unaofuata mwanzo wa dini ya Kikristo (Christian Era) na kuendelea na hadithi hii hata mwisho, huutia moyo nuru. Hivi ni vitabu ambavyo husaidia kuwafanya Waadventista Wasabasto “wana wa nuru” na “wana wa mchana.” Twaona katika jambo hili utimilifu wa ahadi hii:KN 12.5

    “Hakika Bwana Mungu hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”KN 13.1

    Akiandika jinsi nuru ambayo ameielezea katika vitabu hivi vya kisa cha Vita Kuu ilivyomfikia, Ellen White asema : “Kwa njia ya nuru ya Roho Mtakatifu, mambo ya vita ya muda mrefu baina ya mema na mabaya yamefunuliwa kwa mwandishi wa kurasa hizi. Mara kwa mara naliruhusiwa kutazama katika vizazi mbalimbali, kazi ya vita kuu ya Kristo, Mkuu wa uzima, Aliye asili ya wokovu wetu, Shetani, mkuu wa uovu, aliye asili ya dhambi, mwasi wa kwanza wa sheria takatifu ya Mungu ”KN 13.2

    Kadiri Roho wa Mungu alivyonifunulia akilini mwangu maneno makuu ya kweli ya Neno lake, na mambo ya wakati uliopita na ya wakati ujao, nimeamuriwa kuwajulisha wengine mambo yaliyofunuliwa hivi-kufuatisha historia ya vita hivi zamani za kale na, hasa kuvionyesha kwa njia itakayoleta nuru kwenye shindano linalokaribia upesi la wakati ujao.”KN 13.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents