Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuwaelekeza Wanadamu Kwenye Biblia

  Shuhuda zilizoandikwa si za kutoa nuru mpya, bali kutia moyoni kwa nguvu maneno ya kweli yaliyotolewa kwa uongozi wa Roho ambayo yamekwisha kufunuliwa. Wajibu wa mwanadamu kwa Mungu na kwa mwanadamu mwenzake umeelezwa dhahiri katika Neno la Mungu, lakini ni wachache wenu wenye kuitii nuru hii iliyotolewa. Kweli nyingine haikutolewa; ila Mungu kwa njia ya Shuhuda hizi ameyadhihirisha maneno makuu ya kweli ambayo yamekwisha tayari kutolewa na kwa njia aliyochagua yeye mwenyewe akayaleta mbele ya watu kuamsha na kuwatia moyo kwayo, ili wote wasiwe na udhuru wo wote. Shuhuda hizi hazipaswi kulitweza Neno la Mungu, bali kuziinua juu na kuziadilisha akili za moyoni kulifikia, kusudi urahisi mzuri wa Neno la kweli upate kuwavuta wote. 25T 665;KN 106.2

  Roho hakutolewa wala hawezi kupewa watu kutangua Biblia; maana Maandiko Matakatifu husema dhahiri kuwa Neno la Mungu ni kipimo ambacho kwacho mafundisho na mambo yote ya maisha hayana budi kupimwa.... Isaya asema, “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” (Isaya 8:20). 3GC, lntroduction, p. vii;KN 106.3

  “Ndugu J. huzitatanisha akili kwa kujaribu ionekane kana kwamba nuru aliyoitoa Mungu kwa njia ya SHUHUDA hizi ni nyongeza ya Neno la Mungu, lakini kwa kufanya hivi hukosa. Mungu ameona kuwa njia hiyo yafaa kuyaongoza mawazo ya watu wake kwenye Neno lake, ili awafahamishe Neno lake wazi zaidi. Neno la Mungu latosha kuzitia nuru akili zilizoingia giza kabisa na laweza kufahamika na wale aambao wanataka kulifanamu. Lakini ingawa baadhi ya hao, wengine wanaodai kulifanya Neno la Mungu somo lao huonekana wakienenda kinyume cha mafundisho yake yaliyo dhahiri kabisa. Basi, ili kuwaacha wanaume na wanawake pasipo udhuru wawezao kutoa, Mungu hutoa shuhuda dhahiri na nalisi, zenye kuwarudisha kwenye Neno ambalo waliacha kulifuata. Neno la Mungu hufungamanisha kwa jumla kanuni za matengenezo ya mazoea mema ya maisha , na shuhuda hizi, kwa jumla na kwa kila mmoja zimekusudiwa kuwatazamisha zaidi kanuni hizi hasa.KN 106.4

  Naliitwaa Biblia na kuizinga na hizi Shuhuda kwa Kanisa, ambazo zilitolewa kwa ajili ya watu wa Mungu. Hapa nikasema habari za watu karibu wote zaguswa. Dhambi ambazo wanapaswaw kuepukana nazo zimeonyeshwa. Mashauri mema ambayo huyatamani huweza kupatikana hapa, yametolewa kwa ajili ya mambo ya wengine yakiwa na hali ya kuwafaa wao wenyewe pia. Mungu amependezwa kuwapa amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni.KN 107.1

  Lakini si wengi wenu wajuao kwa kweli kila kilichomo ndani ya Shuhuda hizi. Hamyajui Maandiko Matakatifu. Kama mngalilifanya Neno la Mungu somo lenu la kujifunza, mkiwa na moyo wa kutaka kukichunguza kipeo cha Biblia na kupata ukamilifu wa Mkristo, msingehitaji Shuhuda hizi. Kwa sababu mmedharau kukifahamu Kitabu hiki kilichotolewa kwa uongozi wa Roho ndiyo maana Mungu amejaribu kuwapata kwa shuhuda nyepesi na dhahiri, zenye kuwatazamisha maneno yaliyotolewa kwa uongozi wa Roho ambayo mmeacha kuyatii, na kuwasihi kuitengeneza mienendo yetu ipatane na mafundisho yake safi na yaliyo bora. 45T 663665;KN 107.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents