Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Shetani Hawezi Kuingia Moyoni Tusipokubali

    Mungu ametayarisha ili tusije tukajaribiwa kupita tuwezavyo kustahimili, lakini pamoja na kila jaribu atafanya mlango wa kutokea. Kama tukimtii Mungu kabisa, hatutakubali moyo kuyafurahia mawazo ya kujifikiri nafsi wenyewe.KN 189.3

    Pakiwako na njia yo yote ambayo kwayo Shetani aweza kuingia moyoni, atapanda magugu yake na kuyafanya yaote mpaka yatakapotoa mavuno mengi. Kwa vyo vyote Shetani hawezi kuyatawala mawazo, maneno, wala matendo, kama tusipokubali wenyewe kufungua mlango na kumkaribisha. Tukimkaribisha ataingia, na kwa kuifanyia nila mbegu njema iliyokwisha kupandwa moyoni, huyafanya maneno ya kweli yasiwe na matokeo mema.KN 189.4

    Si salama kwetu kuendelea kufikiri habari za manufaa yawezayo kupatikana kwa kuyakubali mashauri ya Shetani. Dhambi ni uasi na balaa kubwa ni kwa kila mtu anayejifurahisha kwayo; lakini hupofusha na kudanganya kwa hali yake, nayo itatuvuta kwa werevu. Kama tukijihatarisna mahali pa Shetam, hatuna ahadi ya kulindwa na uwezo wake. Kwa hiyo ni juu yetu kufunga kila njia ambayo kwayo mshawishi aweza kutufikia.KN 189.5

    Kila Mkristo nana budi kulinda zamu daima, kuangalia kila njia ya rohoni ambamo Shetani aweza kupata upenyo. Yampasa (Mkristo) Kuomba msaada wa Mungu huku akiyapinga kwa uthabiti maelekeo vote ya dhambi. Kwa moyo, kwa imani, kwa jitihada, aweza kushinda. Lakini akumbuke kuwa ili kuupata ushindi Kristo hana budi kukaa ndani yake naye kukaa ndani ya Kristo.KN 189.6

    Kila kitu kiwezacho kufanywa ili kutuweka pamoja na watoto wetu mahali ambapo hatuwezi kuyaona maovu yatendwavo ulimwenguni kingefanywa. Yatupasa kujihadhari sana na macho yetu pamoja na masikio yetu kusudi mambo hayo mabaya yasiingie mioyoni mwetu. Usijaribu kuona jinsi gani uwezavyo kutembea ukingoni mwa jabali bila kuanguka. Epukana na hatari ya kwanza kabisa unayokaribiana nayo. Mambo ya kiroho hayafai kuchezacheza nayo. Mali yako kubwa ni tabia yako. Itunze kama ambavyo ungalitunza hazina ya dhahabu. Uadilifu, kujiheshimu (kuchunga cheo), uwezo mkuu wa kupinga, havina budi kuhifadhiwa kwa nguvu siku zote. Lazima kujihadhari kila wakati; tendo moja la utani, tendo moja lisilo la akili, laweza kuihatarisha roho ya mtu, kuyafungulia majaribu, na kudhoofisha uwezo wa kuyapinga. 1 AH 401-404.KN 190.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents