Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utii ni Wajibu wa Kila Mtu

  Muumbaji wa mwanadamu amepanga mashine hii yenye uhai ya miili yetu. Kila sehemu imefanywa vizuri ajabu na kwa hekima. Mungu ameahidi kuitunza mashine hii ya mwili wa mwanadamu katika hali njema ya afya ikiwa mwanadamu atazitii sheria za Mungu na kushirikiana naye. Kila sheria inayoitawala mashine ya mwili wa mwanadamu ingefikiriwa kuwa takatifu kwa kweli kwa asili, kwa hali, na kwa ukubwa kama lilivyo Neno la Mungu. Kila tendo la kutojali na la uzembe, kuitenda vibaya mashine hii ya ajabu iliyo mali ya Mungu, kwa kutojali sheria zake zilizoelezwa wazi katika mwili wa mwanadamu, ni uasi wa sheria yake Mungu. Twaweza kuona na kuisifu kazi ya Mungu katika viumbe wa asili, lakini mwili wa mwanadamu ndio kitu cha ajabu kabisa. 4CD 17;KN 243.6

  Kwa kuwa kawaida ya vitu vyote ni sheria za Mungu, ni dhahiri kuwa ni wajibu wetu kujifunza sheria hizo kwa uangalifu. Yatupasa kujifunza masharti yake kwa habari za miili yetu wenyewe na kuzitii. Kutojali mambo nayo ni dhambi.KN 244.1

  Wanaume kwa wanawake wakiwa wameongoka kweli kweli, wataziheshimu kwa uaminifu kanuni za maisha ambazo Mungu ameziweka mwilini mwao, hivyo watatafuta kuepukana na udhaifu wa mwili, akili, na tabia ya moyoni. Utii wa sheria hizo hauna budi kufanywa kuwa wajibu umpasao kila mtu. Sisi wenyewe hatuna budi kupatwa na madhara ya kuiasi hiyo sheria. Hatuna budi kutoa habari kwa Mungu kwa ajili ya mazoea na matendo yetu. Kwa hiyo, swali kwetu si, “Walimwengu watasema nini?” Bali, “Nikiwa nadai kuwa ni Mkristo, nitautendeaje mwili niliopewa na Mungu? Je, nitafanya kazi kwa ajili ya ubora wa mambo ya dunia hii na ya kiroho kwa kuutunza mwili wangu kama hekalu akaapo Roho Mtakatifu, ama nitajitia mwenyewe katika mawazo na desturi za walimwengu?” 56T 369, 370;KN 244.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents