Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 14 - Shuhuda kwa Kanisa

    KADIRI mwisho unavyozidi kukaribia na kazi ya kutoa onyo la mwisho kwa walimwengu inavyozidi kuenea, ndivyo linavyozidi kuwa jambo kubwa kwa wale wanaokubali ukweli wa wakati huu kufahamu vizuri hali na mvuto wa Shuhuda hizi, ambazo Mungu kwa majaliwa yake amezifungamanisha na kazi ya ujumbe wa yule malaika wa tatu tokea mwanzo wake hasa.KN 105.1

    Zamani Mungu alisema na wanadamu kwa kinywa cha manabii na mitume. Siku hizi asema nao kwa Shuhuda za Roho wake. Kamwe haujakuwako wakati ambapo Mungu aliwafundisha watu wake kwa moyo wa bidii kuliko anavyowafundisha sasa juu ya mapenzi yake na njia apendayo waifuate.KN 105.2

    Maonyo na maneno ya kukaripia hayatolewi kwa wakosaji miongoni mwa Waadventista Wasabato kwa sababu maisha yao yanastahili kulaumiwa zaidi ya maisha ya watu wengine wanaodai kuwa ni Wakristo wa makanisa mengine bali kwa sababu wanayo nuru kuu, na kwa ungamo lao wametwaa mahali pao kama watu wa pekee, wateule wa Mungu, wenye sheria ya Mungu ikiwa imeandikwa mioyoni mwao.KN 105.3

    Maneno ya ujumbe niliyopewa kwa ajili ya watu mbalimbali mara nyingi nimeyaandika kwa faida yao nikifanya hivi kwa wengi wao walionisihi sana kuwafanyia vile. Kadiri kazi yangu ilivyozidi, hili likawa jambo kubwa na sehemu ya kunichosna ya kazi yangu.KN 105.4

    Katika maono niliyopewa zamani miaka kama ishirini hivi iliyopita (1871) naliamriwa kutoa, kanuni kuu kwa kusema na kuandika na wakati huo huo kueleza hatari, makosa, na dhambi za watu mbalimbali, ili wote wapate kuonywa, kuadilishwa, na kupewa shauri jema. Naliona kuwa wote wangechunguza sana mioyo na mienendo yao wenyewe ili kuona kama hawakufanya makosa yayo hayo kama wengine walioonywa kwa maandishi hayo au kama maonyo yaliyotolewa kwa ajih ya wengine hayakuwahusu wao pia. Kama m hivyo, wangepaswa kuona moyoni kuwa mashauri na maneno ya kukaripia yalitolewa kwa ajili ya wale, nayo yangewafaa na kuwahusu wao kana kwamba yalikuwa yakinenwa kwao hasa.KN 105.5

    Mungu anakusudia kuipima imani ya wote wanaojidai kuwa wafuasi wa Kristo. Ataupima unyofu wa sala za wale wote wanaojidai kuwa wanataka sana kujua wajibu wao. Atadhihirisha wajibu huo. Atawapa wote nafasi kubwa kukuza kile kilichomo mioyoni mwao.KN 105.6

    Bwana hukaripia na kutoa makosa watu wanaojidai kuishika sheria yake. Huonyesha dhambi zao na kudhihirisha uovu wao kwa sababu ataka kuwatenga na dhambi na uovu wote, ili waukamilishe utakatifu kwa kicho cha Bwanaa. Mungu hukaripia, hulaumu na huwatoa makosa kusudi wapate kuadilishwa kutakaswa, kukuzwa, na hatimaye kupandishwa juu kitini pake pa enzi. 15T 654-662;KN 106.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents