Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Heshima ya Kazi

    Yafaa vijana waongozwe kuiona heshima halisi ya kazi za juhudi. Waonyeshwe kwamba Mungu ni mtendaji wa kazi daima. Viumbe wote kwa asili hufanya kazi waliyowekewa. Utendaji umeenea kwa viumbe wote, nasi ili kuitimiza kazi yetu, yatupasa pia kuwa watendaji hodari wa kazi. 34ED.214 ;KN 238.1

    Kazi za juhudi ambazo huunganishwa pamoja na kuzitumikisha akili kwa ajili ya manufaa, ni utawala katika maisha ya manufaa, zikitiwa utamu siku zote na fikara ambazo huustahilisha na kuelimisha akili na mwili vizuri ili kuifanya kazi Mungu aliyowawekea wanadamu kuitenda katika idara mbalimbali za kazi. 35.KN 238.2

    Mtu yeyote kati yetu asiionee kazi haya, hata iwe ni ndogo au ya kitumwa kiasi gam. Kazi ni heshima. Wote wanaofanya kazi, iwe ni kazi ya kichwa au ya mikono, nao waifanyao wakiwa waume au wanawake, ni watenda kazi. Na wote, iwe ni katika kufua nguo au kuosha vyombo vya jikoni, wanafanya wajibu wao na kuitukuza dini yao kwa kiasi kinacholingana barabara na wanapohudhuria katika mikutano. Wakati mikono inapojishughulisha katika kazi zilizo za kawaida sana, akili yaweza kuadilishwa na kukuzwa kwa kuwa na mawazo yaliyo safi na matakatifu. 36FE.229 ;KN 238.3

    Sababu mojawapo iliyo kubwa inayofanya kazi ngumu za juhudi za mwili kudharauliwa ni kutokutengeneza, na kufanywa vibaya mara nyingi. Hufanywa kwa kuwa imebidi tu, wala si kwa hiari. Mtenda kazi hatii moyo kuifanya kazi hiyo, hachungi cheo, wala hapati heshima ya wengine. Mazoea ya kazi za juhudi yangeweza kulisahihisna kosa hili. Hayo yangekuza mazoea ya usahihi na bidii nyingi. 37ED.222 ;KN 238.4

    Ni dhambi kuwaacha watoto kukua kivivu. Hebu wavizoeze viungo vyao na misuli, hata kama inawachosha. Ikiwa hawatumikishwi kupita kiasi, uchovu wawezaje kuwadhuru kuliko unavyokudhuru wewe? Kuna tofauti kabisa baina ya uchovu na ulegevu. Watoto wanahitaji mageuzi ya kazi mara kwa mara na vipindi vya pumziko zaidi kuliko watu wazima wanavyohitaji; lakini iwapo bado ni wachanga, waweza kuanza kujifunza kufanya kazi, na watakuwa na furaha mawazoni mwao kwamba nao waweza kujifanya kuwa wenye manufaa. Usingizi wao utakuwa mtamu baada ya kufanya kazi ya kutia afya, na watakuwa wameburudishwa kwa kazi ya siku itakayofuatia. 38AH.289 ;KN 238.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents