Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Dhambi Isiyosameheka

    Ni nini kifanyacho dhambi juu ya Roho Mtakatifu? Ni kumdhania Shetani kazi ambayo kwa kweli inatendwa na Roho Mtakatifu. Kwa mfano, hebu fikiri kuwa mtu fulani ni shahidi wa kazi ya pekee ya Roho wa Mungu. Analo jambo linaloonyesha kwamba kazi hii ni kazi inayopatana na Maandiko matakatifu, Roho hushuhudia pamoja na roho yake pia kuwa ni kazi ya Mungu. Lakini, baadaye huanguka majaribuni; kiburi, ukinaifu, au tabia nyingine mbaya, humtawala; na akikataa mambo yote yaonyeshayo tabia takatifu ya kazi hiyo, husema kuwa kile ambacho zamani alikuwa akikiri kuwa ni uwezo wa Roho Mtakatifu kilikuwa uwezo wa Shetani. Mungu hufanyia kazi moyo wa binadamu kwa njia ya Roho wake; na watu wanapompinga Roho makusudi na kuitaja kuwa yatoka kwa Shetani, hukata njia ambayo kwayo Mungu huweza kuwasiliana nao. Kwa kulikana jambo ambalo huonyesna kwamba Mungu amependezwa kuwapa, wanaifungia nje nuru ambayo imekuwa iking’aa mioyoni mwao, na matokeo yake huwa kuachwa gizani. Hivyo maneno ya Kristo yanathibitishwa. “Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!” (Mathayo 6:23). Kwa muda, watu waliotenda dhambi hii huenda wakaonekana kuwa watoto wa Mungu; lakini pakitokea hali za mambo ili kuikuza tabia na kudhihirisha kuwa ni watu wenye moyo gani, itaonekana kuwa ni wa yule adui, wakisimama chini ya bendera yake nyeusi. 957634;KN 93.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents