Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 6 - Maisha Matakatifu

    MWOKOZI wetu hudai vyote tulivyo navyo; anataka mawazo yetu ya kwanza yawe matakatifu sana, upendo wa ndani ulio safi kabisa. Kama tu washiriki kwa kweli wa tabia ya Mungu, tutamsifu daima mioyoni mwetu na kwa vinywa vyetu. Usalama wetu tu ni kumtolea vyote tulivyo navyo, na kudumu kukua katika neema na katika kuijua kweli. 118 SL 95;KN 58.1

    Utakaso ulioelezwa katika Maandiko Matakatifu unahusu mwili mzima-moyo, roho, na mwili. Hili ndilo wazo halisi la kujitoa wakfu kabisa. Paulo huomba dua kusudi kanisa la Thesalonike lipate kuufaidi mbaraka huu mkuu. “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo” (1 Wathesalonike 5:23).KN 58.2

    Katika jamii ya watu wa dini, yako mafundisho ya utakaso ambayo ni ya uwongo na ya hatari kwa mvuto wake. Mara nyingi wenye kukiri utakaso huu hawana kitu halisi walichoshikilia. Utakaso wao ni mazungumzo na ibada potovu.KN 58.3

    Huacha kutumia akili na busara, kutegemea hisia zao, wakijenga msingi wa madai yao ya utakaso katika msisimko ambao wamewahi kuupata. Ni wakaidi na wapotoshaji katika kusisitiza kauli za madai yao ya utakatifu, wakitoa maneno mengi, lakini yasiyo na matunda ya thamani kama uthibitisho. Watu hawa wenye kujidai kuwa ni watakatifu licha ya kujidanganya nafsi zao wenyewe kwa maneno yao ya hila, hata hutoa mvuto kuwapotosha wengi ambao hutaka sana kwa uaminifu kutii mapenzi ya Mungu. Wanaweza kusikika wakirudia tena na tena kusema, “Mungu aniongoza, Mungu ananifundisha! Naishi pasipo dhambi!” Wengi wakutanao na roho hii hupambana na giza, jambo wasiloweza kulifahamu. Lakini hilo nailo lililo kinyume hasa cha Kristo, ambaye ni Kielelezo cha kweli peke yake. 2SL 7-10; KN 58.4

    Utakaso ni kazi ya kuendelea daima. Hatua moja moja zimewekwa mbele yetu katika maneno ya Petro: “Mkijitahidi sana wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa, na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.” (2 Petro 1:5-8). “Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu kristo” (mafungu 10:11).KN 58.5

    Hii ni njia ambayo kwayo twaweza kujihakikishia kuwa kamwe hatutaanguka. Wale ambao huufanyia kazi mpango huu wa ongezeko la kuzipata sifa njema za Kristo wameahidiwa kuwa Mungu atatekeleza mpango wa kuwazidishia katika kuwakarimia karama za roho wake. 3SL 94, 95;KN 59.1

    Utakazo si kazi ya punde tu, saa moja au siku moja. Ni kukua daima katika neema. Hatuwezi kujua leo jinsi mashindano yetu yatakavyokuwa magumu kesho. Shetani yu hai, naye ana bidii, na kila siku yatupasa kumlilia Mungu kwa bidii atupe msaada na nguvu ya kushindana naye. Ili mradi Shetani yu kazini tutakuwa na kazi ya kuitiisha nafsi, mashambulio ya kuyashinda, na hakuna kituo, hakuna mahali tuwezapo kuflka tukasema tumefikia mwisho kabisa.KN 59.2

    Maisha ya Mkristo ni kusonga mbele daima. Yesu amekaa kama mtakasaji na msafishaji wa watu wake; na sura yake ikirudishwa ndani yao mithili ya nuru, ni wakamilifu na watakatifu, na walio tayari kuhamishwa kutoka ulimwengu huu. Mkristo anayo kazi kubwa. Tumeonywa kujitakasa na kuachana na uchafu wote wa mwili, na roho, utakatifu kamili katika kicho cha Mungu. Hapa twaona ilipo kazi kubwa. Kuna kazi ya daima kwa Mkristo. Kila tawi katika shina la mzabibu halina budi kutwaa uzima na nguvu kutoka katika mzabibu huo, ili kuzaa matunda. 4IT 340;KN 59.3

    Pasiwepo watu wanaojidanganya wenyewe kwa kuamini kuwa Mungu atawasamehe na kuwabariki wakiwa wanakanyaga mojawapo la masharti yake. Utendaji wa dhambi inayofahamika wa makusuai huinyamazisha sauti ya ushuhuda ya Roho nao huitenga roho ya mtu na Mungu. Ijapokuwa hali ya kujaa furaha ya dini moyoni iwe ya namna gani, Yesu hawezi kukaa katika moyo usiojali sheria ya Mungu. Mungu atawaheshimu wale tu wanaomheshimu. 5SL 92;KN 59.4

    Paulo alipoandika, “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa” (1 Wathesalonike 5:23), hakuwaonya ndugu zake kulenga kwenye kipimo ambacho hawawezi kukifikia; hakuomba kwamba wapate mibaraka ambayo haikuwa mapenzi ya Mungu kuitoa. Alijua kuwa wote ambao wangefanywa wafae kumlaki Kristo kwa amani hawana budi kuwa na tabia safi na takatifu. (Soma 1 Kor. 9:25-27; 1 Kor. 6:19, 20).KN 59.5

    Kanuni ya Mkristo wa kweli haitaacha kupima uzito wa maana ya mambo. Haiulizi, watu watanifikiria nini kama nikifanya jambo hili? Au, Itakuwa na matokeo gani ya baadaye katika maelekeo yangu ya kidunia kama nikifanya hivyo? Kwa tamaa nyingi sana watoto wa Mungu wana hamu kujua angependa wafanye nini, kusudi matendo yao yapate kumtukuza. Mungu ametayarisha mengi ili mioyo na mienendo ya wafuasi wake wote iweze kutawaliwa na neema ya Mungu ili wapate kuwa kama nuru ziwakazo na kung’aa ulimwenguni. 6SL 26, 39;KN 59.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents