Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Umoja Hauna Budi Kutangulia Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu

    Fahamu kwamba ilikuwa baada ya wanafunzi kuwa na umoja kamili, wakati walipokuwa hawakishindanii cheo kikubwa kuliko vyote, hapo Roho alipomwagwa juu yao. Walikuwa na umoja. Hitilafu zote zilikuwa zimeondolewa. Na ushuhuda walioutoa baada ya kumwagiwa Roho ulikuwa mmoja. Angalia neno hili: “Jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja.” (Matendo 4:32) Roho wake Yeye aliyekufa ili wenye dhambi wapate kuishi alihuisha kusanyiko lote la waaminio.28T 20, 21:KN 113.4

    Wale wanafunzi hawakujiombea mbaraka wao wenyewe. Walikuwa wakilemewa na mzigo wa roho za watu. Injili ilikuwa haina budi kuenezwa mpaka mwisho wa dunia, nao walidai karama ya uwezo ambao Kristo alikuwa ameahidi. Kisha ndipo Roho Mtakatifu alipomwagwa, na maelfu wakaongoka kwa siku moja.KN 114.1

    Kadhalika ndivyo inavyoweza kuwa sasa. Hebu Wakristo waache mafarakano yote na kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kukiokoa kilichopotea. Hebu waombe kwa imani moaraka ulioahidiwa, nao utafika. Kumwagiwa Roho katika siku za mitume kulikuwa “mvua ya vuli,” na matokeo yake yalikuwa mazuri. Lakini mvua ya masika itakuwa nyingi zaidi. Je, ahadi gani iliyotolewa kwa wale wanaoishi katika siku hizi za mwisho? “Irudieni ngome, enyi wafungwa wa tumaini; hata hivi leo nasema ya kwamba nitakurudishia maradufu.” “Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni.” (Zekaria 9:12; 10:1).KN 114.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents