Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    “Msiwiwe na Mtu Cho Chote”

    Watu wengi walio maskini ni maskini kwa sababu hutumia fedha zao mara tu wazipatapo. Kuchukua na kutumia fedha kwa kusudi lo lote, kabla ya Kustahili kuipata kwa kazi, ni mtego. 3AH 392;KN 176.1

    Ulimwengu una haki kutazamia uaminifu kabisa kwa wale wanaodai kuwa ni Wakristo wa Biblia. Kwa kutojali kwa mtu mmoja kulipa haki yake apaswavyo watu wetu wote wamo katika hatari ya kunesabiwa kuwa si waaminifu. Wale wanaojidai kwa hali yo yote kuwa wenye utauwa, yawapasa kujivika mafundisho wanayoyakiri, wala wasitoe nafasi kwa Neno la Mungu kutukanwa kwa sababu ya mwenendo wao wa kutojali. Mtume asema, “Msiwiwe na mtu cho chote.” 45 T 179-182;KN 176.2

    Wengi, naam, wengi sana, hawajajifunza kwamba wanaweza kupunguza gharama ya matumizi yao isizidi mapato yao. Hawajifunzi kuchukuliana na hali ya mambo yalivyo, nao hukopakopa na kulemewa na madeni, hatimaye hukata tamaa na kuvunjika moyo. 5AH 374;KN 176.3

    Yawapasa kuona kuwa mtu hayafanyi mambo yake kwa njia itakayomwingiza katika deni. Mtu akiwa na deni, yuko katika mmojawapo wa mitego ya Shetani, anayotumia kuzitega roho za watu. Kusudia kutokuwa na deni hata kidogo. Jinyime vitu elfu kuliko kuingia deni. Epukana na deni kama ungaliepukana na ugonjwa wa ndui. 6392, 393;KN 176.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents