Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hatari Katika Kuchelewa

    Katika njozi za usiku maono ya ajabu sana yalipita mbele yangu. Naliona mpira mkubwa sana wa moto ukianguka miongoni mwa majumba mazuri, na kuleta uharibifu wao ghamla. Nalisikia mmoja akisema: “Tulijua kuwa hukumu za Mungu zitakuja juu ya nchi, lakini hatukujua kwamba zingekuja upesi hivi.” Wengine, kwa sauti za maumivu makali, wakasema: “Mlijua! Mbona basi hamkutuambia? Sisi hatukujua.” Kila upande nikasikia maneno ya lawama yakisemwa.KN 77.1

    Kwa wasiwasi mwingi nikaamka. Nikashikwa na usingizi tena, nami nikawa kana kwamba nimo katika mkutano mkubwa. Mkuu mmoja akawa anasema na kundi la watu, ambaye mbele yake palikunjuliwa ramani ya ulimwengu. Akasema kuwa ramani hiyo llionyesha shamba la Mungu la mizabibu, ambalo halina budi kupaliliwa. Kadiri nuru kutoka mbinguni inavyomzukia mtu awaye yote, mtu huyo hupaswa kuitupa kwa wengine. Taa zilikuwa hazina budi kuwashwa mahali pengi, na kutoka katika taa hizi zingine tena zilipaswa kuwashwa.KN 77.2

    Maneno haya yakasemwa mara nyingi: “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali juu ya kiango; nayo yawaangaza wote waliomo nyumbani. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” Mathayo (5:13 - 16). .KN 77.3

    Kila siku ipitayo hutuleta karibu zaidi na mwisho. Je, hutuleta pia karibu na Mungu? Je tunakesha katika kuomba? Wale ambao tunashirikiana nao siku kwa siku huhitaji msaada wetu, na uongozi wetu. Huenda wakawa katika hali ya moyo ambao neno moja kwa wakati wake litaingizwa moyoni na Roho Mtakatifu kama msumari mahali palipo imara. Kesho baadhi ya watu hawa waweza kuwa mahali ambapo kamwe hatutaweza kuwafikia tena. Je mvuto wetu ni wa aina gani kwa hawa wasafiri wenzetu? Twafanya jitihadi gani kuwaongoza kwa Kristo? 9 9727, 28;KN 77.4

    Maadam malaika wanazishikilia zile pepo nne, yatupasa kufanya kazi kwa uwezo wetu wote. Yatupasa kuchukua ujumbe wetu bila kuchelewa hata kidogo. Yatupasa kuonyesha wenyeji wa mbinguni, na wanadamu katika kizazi hiki kilichoharibika tabia, kuwa dini yetu ni imani na uwezo ambao Kristo ndiye Asili yake nalo neno lake ni maneno yaliyosemwa na Mungu. Roho za wanadamu zinaning’inia juu ya mizani. Watakuwa ama raia wa ufalme wa Mungu ama watumwa wa utawala wa Shetani. Wote wanapaswa kuwa na majaliwa ya kushikilia tumaini lililowekwa mbele yao katika Injili, nao wawezaje kusikia pasipo mhubiri? Wanadamu wanahitaji kufanywa upya tabia za moyoni, matayarisho ya tabia, ili wapate kusimama mbele za Mungu. Ziko roho za watu zilizotayari kupotea kwa sababu ya makosa ya kinadharia yanayoenea kila mahali, na ambayo hukusudiwa kuupinga ujumbe wa Injili. Nani ambao sasa watajitoa wakfu-kabisa kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu? 10 6T21;KN 77.5

    Leo sehemu kubwa ya wale ambao ni jumuia yetu ni wafu katika makosa na dhambi. Huja na kwenda kama mlango juu ya bawabu zake. Kwa miaka mingi wamesikiliza na kupendezwa na maneno ya kweli, mazito sana, yenye kuamsha moyo, lakini hawakuyatumia maishani. Kwa hiyo, wamezidi kupungua kuijua thamani ya Neno la Mungu. Maneno yanayogusa ya makaripio na maonyo hayawaamshi kutubu. Nyimbo tamu kabisa zitokazo kwa Mungu kwa njia ya midomo ya wanadamu-kuhesabiwa haki kwa imam, na haki ya Kristo-haviamshi kutoka kwao jibu la upendo na shukrani. Ijapokuwa tajiri wa mbinguni huweka mbele yao vitu vva thamani vya imani na upendo, ingawa huwaalika kununua kutoka kwake “dhahabu iliyosafishwa kwa moto,” na “mavazi meupe” wapate kuvaa, na “dawa ya macho” wapate kuona, huifanya migumu mioyo yao juu yake, na kukosa kubadili uvuguvugu wao kwa upendo na moyo wa bidii. Huku wakifanya ungamo, huzikana nguvu za utauwa. Kama wakiendelea katika hali hii, Mungu atawakataa. Wanajifanya wenyewe wasifae kuwa watu wa nyumba ya Mungu. 11 67426, 427;KN 78.1

    Hebu washiriki wa kanisa wakumbuke kwamba ukweli kuwa majina yao yameandikwa katika vitabu vya kanisa si jambo litakalowaokoa. Hawana budi kujionyesha kuwa wamekubaliwa na Mungu, watenda kazi wasio na sababu ya kutahayari. Siku kwa siku wanapaswa kujenga tabia zao kupatana na maongozi ya Kristo. Wanapaswa kukaa ndani yake, daima wakitumia imani ndani yake. Hivyo watakua mpaka wawe wanaume na wanawake wenye kukifikia cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo-safi wachangamfu, Wakristo wazuri, wenye kuongozwa na Mungu katika nuru lzidiyo kuwa kubwa daima. Kama hayo si mambo yanayoonekana kwao, watakuwa miongoni mwa wale ambao sauti zao siku moja zitapaazwa kwa kuomboleza kwa uchungu: “Mavuno yamepita, kiangazi kimekwisha, na roho yangu haikuiokolewa! Mbona sikukimbilia kwenye Ngome kujisalimisha! Kwa nini nilichezacheza na wokovu wa roho yangu, na kuipinga roho ya neema?” 12 9748;KN 78.2

    Ndugu na dada mnaodai kuwa mmeliamini neno la Mungu muda mrefu, nawauliza kila mmoja wenu, ‘Je matendo yenu yanapatana na nuru, majaliwa, na nafasi mlizokarimiwa na Mungu?’ Hili ni swali zito lenye maana sana. Jua la Haki amelizukia kanisa na ni wajibu wa kanisa kuangaza. Kila mmoja amejaliwa kukua. Wale wenye uhusiano na Kristo watakua katika neema na katika kumjua Mwana wa Mungu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu cha wanaume na wanawake. Kama wote wanaodai kuliamini neno la Mungu wangetumia kwa faida uwezo wao na nafasi zao kujifunza na kutenda, wangeweza kuwa wenye nguvu katika Kristo. Si neno kazi yao ya maisha iwe ya namna gani,-wakiwa wakulima, mafundi wa mashine, walimu au wachungaji wa makanisa,kama wakiwa wamejitoa kabisa wakfu kwa Mungu watakuwa watenda kazi hodari kwa Bwana wa mbinguni. 13 67423;KN 78.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents