Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kupenda Kujifunza Biblia Si Jambo la Kawaida

    Wazee na vijana pia hudharau Biblia. Hawaifanyi somo lao la kujifunza, kanuni ya maisha yao. Hasa vijana ndio wenye kosa hili la kuidharau. Wengi wao wanapata nafasi kusoma vitabu vingine, lakini kitabu hiki chenye kuelekeza njia iendayo uzimani hakisomwi kila siku. Hadithi zisizofaa husomwa kwa bidii, huku Biblia ikidharauliwa. Kitabu hiki ni kiongozi wetu kwa maisha bora zaidi, na matakatifu zaidi. Vijana wangekitaja kuwa kitabu cha kupendeza sana walichopata kusoma kama akili zao zisingalipotoshwa na kule kusoma hadithi za uongo. 9CT 138, 139;KN 102.2

    Kama watu waliopata nuru kuu, yatupasa kuwa wenye kuinua hali katika mazoea yetu, katika maneno yetu, katika maisha yetu ya nyumbani na katika jamaa. Lipe Neno la Mungu hadhi cnake kama kiongozi nyumbani. Hebu lihesabiwe kama mshauri katika kila shida, kanuni ya kila kazi. Je, ndugu na dada zangu watasadikishwa kuwa kamwe hapawezi kuwapo mafanikio halisi kwa mtu awaye yote nyumbani lsipokuwa kama neno la kweli la Mungu hekima ya haki litawaongoza? Jitihadi zote zingefanywa na akina baba na mama kujibiidisha na kuacha mazoea ya uvivu ya kuihesabu kazi ya Mungu kama mzigo. Uwezo wa Neno la kweli la Mungu hauna budi kuwa njia ya kutakasa nyumbani. 10CG 508, 509;KN 102.3

    Katika miaka yao ya kwanza watoto yawapasa kufundishwa madai ya sheria ya Mungu na imani kwa Yesu Mwokozi wetu inayosafisha mawaa ya dhambi. Imani hii haina budi kufundishwa siku kwa siku kwa mafundisho na kielelezo. 115T 329;KN 102.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents