Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vipimo Vya Kufaa Kwa Nabii wa Kweli

    Pamoja na vipimo hivyo vya Biblia, Mungu ametoa shuhuda zinazodhinirisha kuwa kazi hii ni ya maongozi yake. Miongoni mwa hayo ni:KN 34.2

    1. Wakati unaofaa wa ujumbe huu. Watu wa Mungu wamo katika mahitaji maalumu, na ujumbe huu huwajia wakati hasa wanapouhitaji kuyatimiza mahitaji hayo, kama vile ilivyokuwa njozi ya kwanza aliyopewa Ellen White.KN 34.3

    2. Hali ya kufaa ya ujumbe huu. Habari zilizofunuliwa kwa Ellen White katika njozi zilikuwa za thamani kuu, zenye kukidhi hitaji kubwa. Angalia jinsi ambavyo maonyo ya ushuhuda huu yaingiavyo kwa njia ya kufaa katika maisha yetu ya kila siku.KN 34.4

    3. Uzuri wa kiroho wa maneno ya ujumbe huu. Hayasemi mambo ya kitoto au ya kawaida, bali mambo makubwa yenye maana. Lugha yenyewe ni bora sana.KN 34.5

    4. Namna njozi hizi zilivyotolewa. Nyingi miongoni mwa njozi hizi ziliambatana na maajabu yaliyoonekana kwa macho kama ilivyoelezwa katika utangulizi huu. Mambo yaliyompata Ellen White katika njozi yalikuwa sawa na yale ya manabii wa Biblia. Hiki, ingawa si kipimo, lakini ni mojawapo ya mambo mengine yamshuhudiayo.KN 34.6

    5. Njozi zilikuwa mambo halisi, siyo maono tu. Katika njozi, Ellen White aliona, akasikia, na kupokea maagizo kutoka kwa malaika. Njozi hizi zisingeweza kuhesabiwa kuwa zatokana na mambo ya kuhamakisha au ya kudhaniwa tu.KN 34.7

    6. Ellen White hakushawishiwa na wale waliomzunguka. Alimwandikia mtu mmoja: “Unadhani watu wameongoza mafikara yangu, lakini nikiwa katika hali hii sifai kuaminiwa katika kazi ya Mungu.”KN 34.8

    7. Kazi yake ilishukuriwa na watu wa hirimu au rika yake. Wale waliokuwa kanisani waliokaa na kufanya kazi pamoja na Ellen White, na wengi nje ya kanisa walimfahamu Ellen White kama “mjumbe wa Mungu” kweli kweli. Wale waliokuwa karibu sana naye walikuwa na imani kubwa sana katika mwito na kazi yake.KN 35.1

    Vipimo hivi vinne vya Biblia na mambo haya dhahiri ambayo Mungu amewapa watu wake ili wapate kuwa na imani katika ujumbe huu na mjumbe huyu hutuhakikishia kuwa kazi hii ni ya Mungu nayo haistahili kutiliwa mashaka.KN 35.2

    Vitabu vingi vya Ellen G. White vimejaa maonyo na mafundisho yenye thamani daima kwa kanisa. Ingawa shuhuda hizi zilikuwa za namna iliyopasa watu wote kwa jumla ama shuhuda za pekee kwa jamaa au kwa mtu mmoja mmoja lakini zinatufaa hata siku hizi. Juu ya jambo hili, Ellen White anasema:KN 35.3

    “Kwa sababu maonyo na mafundisho yaliyotolewa katika shuhuda hizi kwa ajili ya watu mmoja mmoja huwahusu na kuwa na nguvu ile ile kwa wengine wengi ambao hawakuonyeshwa hasa kwa njia hii, ilionekana kuwa wajibu wangu kuchapisha shuhuda hizi za mtu mmoia mmoja kwa ajili ya faida ya kanisa Sijui njia nyingine iliyo bora zaidi kutoa maoni yangu juu ya hatari na makosa ya watu wote na wajibu wa wote wampendao Mungu na kuzishika amri zake, kuliko kwa kuzitoa shuhuda hizi.”KN 35.4

    Ni kosa kutumia vibaya shuhuda hizi kwa kuzisoma ili kuona mahali pa kumhukumu ndugu mwenzako. Kamwe shuhuda hizi zisitumiwe kama rungu kuwalazimisha ndugu wa kiume au wa kike kuona mambo ambayo hayana budi kuachwa kwa mtu kuyamaliza mwenyewe na Mungu.KN 35.5

    Maonyo haya yangesomwa ili kupata kanuni kubwa ambazo huyahusu maisha yetu siku hizi. Baadhi ya maneno ya ujumbe huu yalitolewa kama maonyo au makaripio kwa wakati fulani maalum au mahali fulani maalum, lakini kanuni zilizoelezwa ni zenye kuhusu po DOte kwa maana yake na wakati zinapotumiwa. Moyo wa mwanaaamu ni hali moja ulimwenguni mwote; shida za mmoja mara nyingi ni shida za mwingine. Ellen White ameandika, “Katika kuyakaripia makosa ya mtu, Mungu amekusudia kuwatoa makosa wengi.” “Huyadhihirisha makosa ya wengine ili wengine wapate kuonywa kwa njia hiyo.” Karibu na mwisho wa maisha yake Ellen White alitoa ushauri huu ufuatao:KN 35.6

    “Kwa njia ya Roho wake Mtakatifu sauti ya Mungu imetujia daima kuonya na kufundisha Muda na mashindano havikuy-atambua mafundisho yaliyotolewa Mafundisho ambayo yali-tolewa siku ya mwanzo wa ujumbe huu hayana budi kushikwa kama mafundisho salama kufuatwa katika siku hizi za mwisho wake.” KN 35.7

    Maonyo ambayo yanafuata yametwaliwa kutoka katika vitabu kadha wa kadha vya Ellen G. White-lakini zaidi sana kutoka katika vile vitabu vitatu vya The Testimony treasures, ambavyo ni muhtasari wa nakala za The Tesmonies for the Church-nayo nutoa mafimdisho yaliyofikiriwa kuwa yenye manufaa makubwa sana kwa kanisa mahali ambapo uchache wa hesabu ya washiriki wa kanisa huzuia isiwezekane kuchapisha kitabu kimoja cha ukubwa wa wastani. Kazi ya kuyachagua na kuyapanga mashauri haya ilifanywa na kamati kubwa, ikifanya kazi kwa ldhini ya Wadhamini wa Vitabu vya Ellen G. White ambayo ilihesabiwa kuwa kazi yao kutunza na kueneza matumizi ya mashauri ya Roho ya Unabii. Uchaguzi mara nyingi huwa mfupi na huwa na kikomo katika mafiindisho makubwa ya kufaa, na hivyo mafundisho mengi ya namna mbalimbali huwamo.KN 36.1

    “Mwaminini Bwana, Mungu wenu, ndivyo mtakavyothibitika; waaminini manabii wake, ndivyo mtakavyofanikiwa.” (2 Mambo ya Nyakati 20:20).KN 36.2

    Wadhamini waKN 36.3

    MAANDISHI YA ELLEN G. WHITE

    Washington, D.C.

    Julai 22, 1957.

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents