Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maoni ya Moyoni Peke yake si Jambo Lionyeshalo Utakaso

  Kuona furaha au kukosa raha si jambo lenye kuonyesha kuwa mtu ametakaswa au hakutakaswa. Hakuna utakaso wa ghafiila. Utakaso wa kweli ni kazi ya kila siku, inayoendelea kadiri maisha yanavyoendelea mpaka mwisho. Wale wanaopigana na majaribu ya kila siku, wakishinda mivuto yao wenyewe ya dhambi, na kutafuta utakatifu wa moyo na maisha, hawajisifii utakatifu. Wanayo njaa na kiu ya haki, Dhambi huonekana kwao kuwa kitu kibayamno. 16SL 10; 2TT 91-94;KN 65.2

  Mungu hatuachi kwa sababu ya dhambi zetu. Pengine twafanya makosa na kuihuzunisha Roho yake; lakini tukitubu, na kumwendea kwa mioyo inayosikitaka kwa ajili ya makosa, hatatufukuza. Viko vipingamizi ambavyo havina budi kuondolewa. Maoni mabaya yametunzwa moyoni, kuna kiburi majivuno, kukosa saburi, na manung’uniko. Hayo yote hututenga na Mungu. Dhambi hazina budi kuungamwa, hapana budi pawepo kazi yenye kina ya neema moyoni. Wale wenye kujiona dhaifu na wenye kukata tamaa waweza kuwa watu hodari wa Mungu, na kufanya kazi bora kwa Bwana. Lakini hawana budi kufanya kazi kwa kiwango cha juu; wamepaswa kutovutwa na moyo wa kujifikiri waonekane.KN 65.3

  Wengine huelekea kuona moyoni kwamba hawana budi kuwa muda wa kuangaliwa waonekane kama wanafaa au hawafai, na kwamba hawana budi kuthibitisha kwa Bwana kuwa wameongoka, kabla hawajaweza kudai mbaraka wake. Lakini watu hawa wenye thamani waweza kudai mbaraka wake hata sasa. Yawapasa wawe na neema yake. Roho wa Kristo, kuwasaidia udhaifii wao, ama sivyo hawawezi kukuza tabia ya Kikristo. Yesu anapenda tumwendee, hivi tulivyo-wenye dhambi, wadhaifu, wasiojitegemea.KN 65.4

  Kutubu, na msamaha pia ni kipawa cha Mungu kwa njia ya Kristo. Ni kwa njia ya mvuto wa Roho Mtakatifu anayetusadikisha hatia ya dhambi, na kuiona haja yetu ya msamaha. Wenye masikitiko kwa ajili ya makosa, wala si wengine, hao ndio wanaosamehewa; lakini neema ya Mungu ndiyo inayoufanya moyo kuwa wenye kutubu. Anajua udhaifu wetu wote na upungufu, naye atatusaidia. 17SL 89-96.KN 66.1

  Giza na mambo ya kukatisha tamaa wakati mwingine vitakuja moyoni na kutuogofya kutuangamiza, lakini haitupasi kutupilia mbali ujasiri wetu. Yatupasa kumkazia Yesu macho, tukiwa tunaona hivyo moyoni, ama tukiwa hatuoni hivyo. Yatupasa kutafuta kufanya kwa uaminifu kila wajibu tujuao na kisha kutegemea kwa utulivu ahadi za Mungu.KN 66.2

  Wakati mwingine kujua sana hali yetu ya kutokustahili kutatia hofu moyoni, lakini hili si jambo la kuonyesha kuwa Mungu amebadilika kwetu, na kutuacha, au sisi tumemwacha Mungu. Hakuna jitihada zo zote ziwezazo kufanywa kuutawala moyo hata kuweza kuvutwa kwa urahisi kuona furaha. Pengine hatuoni leo amani na raha ambayo tuliiona jana; yatupasa kwa imani kushika mkono wa Kristo, na kumwamini kabisa gizani kama nuruni.KN 66.3

  Kwa imani tazameni taji walizowekewa wale ambao watashinda; sikilizeni wimbo wa shangwe wa wale waliookoka. Astahili, astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa na ametukomboa kwa Mungu! Jaribuni kuyahesabu mambo haya kama ni ya hakika.KN 66.4

  Kama tungeruhusu akili zetu kumfikin zaidi Kristo na jamii ya wale wa mbinguni, tungepata kitu cha kututia nguvu na kutusaidia katika kupigana vita vya Bwana. Kiburi na kuipenda dunia vingekosa nguvu kadiri tunavyotafakari utukufu wa ile nchi nzuri ambayo karibuni sana itakuwa makao yetu. Kwa uzuri wa Kristo mivuto yote ya kidunia itaonekana kuwa haina thamani hata kidogo.KN 66.5

  Ijapokuwa Paulo mwishowe alifungwa gerezani Rumikuzuiwa asipate nuru na hewa ya mbinguni, kutengwa na kazi zake alizozitenda kwa bidii kuhubiri Injili, na kutazamia kwa muda kuhukumiwa kufa-lakini hakukubali kushindwa na mashaka au kukata tamaa. Kutoka katika lile gereza lenye giza lilitoa ushuhuda wake wa kufa, uliojaa imani na moyo mkuu ambao umeitia nguvu mioyo ya watakatifu na wafia dini katika vizazi vyote vya baaaaye. Maneno yake yanaeleza vizuri matokeo ya ule utakaso ambao tumejaribu kueleza katika kurasa hizi “Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” (2 Tim. 4:6-8). KN 66.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents