Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 26 - Mivuto ya Kiroho Nyumbani

  Twaweza kupata wokovu wa Mungu nyumbani mwetu; lakini hatuna budi kuuamini, kuushika maishani mwetu, na kuwa na imani idumuyo daima, na kumtumainia Mungu. Amri ambazo Neno la Mungu hututolea ni kwa faida yetu wenyewe. Hutuongezea furaha ya watu wa nyumbani mwetu, na ya wote wanaotuzunguka. Huadilisha tamaa yetu, kuzitakasa akili zetu za kuchagua mazuri, na kuleta amani ya moyoni, na mwisho, uzima wa milele. Malaika wahudumuo watakaa zaidi kwetu, na kupeleka mbinguni habari za maendeleo yetu mema katika maisha ya dini; naye malaika mwandishi ataandika habari nzuri za kupendeza.KN 172.1

  Roho ya Kristo itakuwa mvuto wa daima katika maisha ya nyumbani. Kama wanaume na wanawake watafunua mioyo yao kupokea mvuto wa mbinguni wa kweli na upendo, mafundisho haya yatamiminika tena kama vijito vya maji jangwani, yakiwaburudisha wote na kupaneemesha manali ambapo sasa ni jangwa tupu lisilo na kitu. 1 CG 484; KN 172.2

  Kudharau dini ya nyumbani, kutojali kuwafundisha watoto wenu, ni jambo lisilompendeza Mungu hata kidogo. Kama mmojawapo wa watoto wenu angetumbukia mtoni, na awe anashindana na mawimbi na kuwa katika hatari ya kuzama, ungekuwa na msukosuko wa jambo la kufanywa haraka namna gani! Jitihada kubwa kama nini zingefanywa-sala za namna gani zingeombwa, na bidii kubwa kama nini ingeonyeshwa, kuyaokoa maisha ya mtu huyo! Lakini hapa kuna watoto wenu nje ya Kristo, roho zao hazijaokoka. Pengine ni wakorofi na wasio na adabu, aibu kwa jina la Waadventista. Hupotea pasipo kuwa na tumaini wala Mungu ulimwenguni, nanyi hamjali.KN 172.3

  Snetani hujitahidi sana kuwapotosha watu ili wakae mbali na Mungu; naye hulitimiza kusudi lake wakati maisha ya dini yanapotoswa kwenye shughuli za kazi, wakati anapozishika sana fikara zao katika kazi za uchumi hata wasiwe na nafasi tena ya kusoma Biblia zao, kusali faraghani na kutoa shukrani na kumsifu Mungu kama sadaka ya kuteketeza juu ya madhabahu asubuhi na jioni. Wachache kama mni hufahamu hila za adui mkuu! Wengi kama nini hawazijui hila zake! 257424, 426; KN 172.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents