Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jifunzeni kwa Bidii na kwa Utaratibu

    Wazazi kama mkitaka kuwafundisha watoto wenu kumtumikia Mungu ifanyeni Biblia kuwa kitabu chenu cha mafundisho. Inafunua hila za Shetani. Ni kitu kikubwa chenye kuliinua taifa, cha kugombeza na chenye kutoa makosa ya tabia ya moyoni, kitu cha kuvumbulia ambacho hutuwezesha kupambanua baina ya kweli na uongo. Lo lote lifundishwalo nyumbani au shuleni, Biblia, ikipewa nafasi hii Mungu hutukuzwa, naye atawafanyia kazi katika kuwaongoa watoto wenu. Kuna shimo la mali ya kweli na uzuri katika hiki Kitabu Kitakatifu, na wazazi yawapasa kujilaumu wenyewe kama wasipokifanya kuwa cha kuwapendeza kabisa watoto wao. 55T 322;KN 100.3

    “Imeandikwa” peke yake ilikuwa ndiyo silaha ambayo Kristo alitumia wakati mshawishi alipokuja na hila zake. Kufundisha ukweli wa Biblia ni kazi kuu na ya maana ambayo kila mzazi anapaswa kuifanya. Kwa moyo mzuri, wa furaha uyaweke maneno ya kweli kama yalivyosemwa na Mungu mbele ya watoto. Kama baba na mama, mwaweza kuwa mfano wa mafundisho kwa watoto katika maisha ya kila siku kwa kutumia uvumilivu, huruma, na upendo, kwa kuwavuta kwako. Msiwaache kufanya wapendavyo, lakini waonyesheni kuwa kazi yenu ni kulifuata Neno la Mungu na kuwalea katika malezi na maonyo ya Bwana.KN 100.4

    Shikeni utaratibu katika kujifunza Biblia na watu wa nyumbani mwenu. Heri kutojali kitu cho chote kingine cha kidunia ambacho chadumu muda kitambo tu, .. Ila hakikisheni kuwa roho inalishwa mkate wa uzima. Haiwezekani kukadiria matokeo mema ya saa moja au hata ya nusu saa kila siku inayotolewa wakfu kwa moyo wa furaha, na kutumiwa na watu wote kwenye Neno la Mungu. Ifanye Biblia kuwa yenye kujieleza yenyewe, ukiwakusanya pamoja wote ambao husemekana kuwa wenye kuhusikana na somo lililotolewa nyakati mbalimbali na kwa mambo ya namna mbalimbali. Usivunje darasa lako la nyumbani kwa ajili ya watu wajao kuamkia au wageni. Kama wakifika wakati wa somo hili, wakaribishe walishiriki. Acha ionekane kuwa unauthamini zaidi ujuzi wa Neno la Mungu kuliko mapato ya faida au anasa za dunia. Kama tungejifunza Biblia kwa bidii na kwa kumwomba Mungu sana kila siku, tungeona kila siku ukweli mzuri katika nuru mpya, dhahiri, na yenye nguvu. 6Cg 510, 511KN 100.5

    Yakupasa kuifanya Biblia kuwa kiongozi wako kama ukipenda kuwalea watoto wako katika malezi na maonyo ya Bwana. Hebu maisha na tabia ya Kristo itolewe kama kielelezo kizuri kwao kukiiga. Kama wakifanya kosa, wasomee kile ambacho Mungu alisema juu ya dhambi za namna hiyo. Panatakikana uangalifu wa daima na bidii katika kazi hii. Tabia moja mbaya iliyovumilika na wazazi, isiyosahihishwa na walimu, yaweza kuifanya tabia yote ya mtu kuwa mbaya na isiyo imara. Awafundishe watoto kuwa yawapasa wawe na moyo mpya; ya kuwa akili mpya za kupambanua mazuri hasa, hazina budi kufanyika ndani yao, na nia mpya kutiwa moyoni. Hawana budi kupata msaada kutoka kwa Kristo; hawana budi kuifahamu tabia ya Mungu kama ilivyofunuliwa katika Neno lake. 7CG 515;KN 101.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents