Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuonyesha Tabia ya Mungu kwa Maisha ya Kuwafikiria Wengine Kuliko Mwenyewe Binafsi

    Dhambi ambayo inapendwa sana, na ambayo hututenga na Mungu na kuleta magonjwa mengi ya kiroho yenye kuambukiza, ni choyo (kujifikiria naisi mwenyewe bila kujali wengine). Hapawezi kuwapo kumrudia Bwana isipokuwa kwa kujikana nafsi. Sisi wenyewe hatuwezi kufanya lo lote; lakini, Mungu akitujalia nguvu, twaweza kuishi na kutenda mema kwa wengine, na kwa njia hii kuepukana na uovu wa choyo. Hatuhitaji kwenda nchi za washenzi kuudhihirisha moyo wetu wa kutoa vyote wakfu kwa Mungu katika maisha ya kuwafaidia wengine na ukarimu. Yatupasa kulitenda hili nyumbani, kanisani, miongoni mwa wale tunaoshirikiana nao na ambao tunahusiana kazini. Papo hapo katika maisha ya kawaida ndipo nafsi ipaswapo kukanwa na kutiishwa. Paulo aliweza kusema: “Ninakufa kila siku” Kufa kila siku kwa nafsi katika matendo madogo ya maisha ndiko kunakotufanya washindaji. Yatupasa kujisanau nafsi katika kutaka kuwatendea mema wengine. Wengi wanapungunkiwa sana na upendo kwa wengine. Badala kufanya kazi yao kwa uaminifu, hujaribu kujipendeza nafsi zao wenyewe.KN 92.3

    Mbinguni hakuna ye yote atakayejifikiria nafsi mwenyewe, wala kutafuta kujipendeza nafsi mwenyewe; bali wote, kwa upendo wa kweli na safi, wataitafuta furaha ya wenyeji wa mbinguni pande zote kuwazunguka. Kama tukipenda kuifaiai hali ya mbingum katika nchi mpya, hatuna budi kutawaliwa hapa na kanuni za mbinguni. 72T 132, 133;KN 93.1

    Nalionyenswa kwamba pamekuwako kujipima kupita kiasi sisi kwa sisi, tukiwatwaa wanadamu wenye kufa kuwa mfano, hali tukiwa na kielelezo amini, asiyekosea. Haitupasi kujilinganisha na walimwengu, wala na mawazo ya wanadamu, wala na vile tulivyokuwa zamani kabla ya kulipokea Neno la Mungu. Lakini imani na cheo chetu ulimwenguni, kama ilivyo sasa hakina budi kulinganishwa na kile tungalichokuwa kama mwenendo wetu ungekuwa umeendelea daima mbele na juu kwa kuwa tumejidai kuwa wafuasi wa Kristo. Huu tu ndio ulinganifu wa sala uwezao kufanywa. Kwa kila mmoja wa wengine wote itakuwa ni kujidanganywa. Kama tabia ya moyoni na hali ya kiroho ya watu wa Mungu hailingani na mibaraka, majaliwa, na nuru ambayo wamejaliwa kuwa nayo, wanapimwa kwa mizani, na malaika hutoa ripoti, WAMEPUNGUA. 81T 406;KN 93.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents