Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 37 - Elimu ya Kikristo

  TUNAKARIBIA kwa haraka wakati wa hatari za mwisho wa historia ya ulimwengu huu, na ni bora tukifahamu kuwa faida ya elimu itolewayo na shule zetu haina budi kuhitilafiana na ile ya shule za kidunia. 1CT 56;KN 229.1

  Mawazo yetu juu ya elimu ni kidogo sana na shabaha yetu iko chini sana. Kuna haja ya cheo cha juu, na shabaha bora zaidi. Maana ya elimu ya kweli siyo mfululizo wa mafundisho fulani tu, la, bali ma maana zaidi ya kujitayarisha kwa ajili ya maisha haya ya sasa. Huhusu mwili mzima wa mtu, muda wote wa maisha yake awezayo kuishi. Ni kukua kunakopata na mwili, akili na nguvu za kiroho. Humtayarisha mwanafunzi kwa ajili ya furaha ya kazi ulimwenguni humu na kwa ajili ya furaha bora zaidi ya kazi kubwa zaidi katika ulimwengu ujao. 2Ed.13;KN 229.2

  Maana halisi ya kazi ya elimu na ile ya kazi ya ukombozi ni moja; kwa kuwa elimu, kama ilivyo na ukombozi “msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani Yesu Kristo.” 3Ed.30;KN 229.3

  Kumrudisha binadamu apatane na Mungu, hata kumkuza na kumwadilisha moyoni mwake ili aweze tena kurudisha sura ya Muumbaji, ndilo kusudi kubwa la elimu na malezi yote ya maisha. Hii ilikuwa kazi ya maana sana hata ikamfanya Mwokozi ayaache makao ya mbinguni na kuja ulimwenguni humu katika hali ya mwili wa kibinadamu, Kusudi apate kuwafundisha watu jinsi ya kupata hali ya kufaa kwa maisha yale bora zaidi ya juu. 4 CT.49;KN 229.4

  Ni vyepesi zaidi kuingia polepole katika mipango na desturi za kidunia, bila kujua, na kusahau habari za wakati nasa tunamoishi, au kutofikiri kazi kubwa ipasayo kumalizwa, kuliko walivyokuwa watu wa siku zile za Nuhu. Kuna hatari daima kwa walimu wetu kwenda njia ile ile ya Wayahudi, na kufuata desturi, mazoea, na mapokeo ya wazee wao ambayo hayakutolewa na Mungu. Wengine hushikilia sana desturi za zamani na mafundisho mbalimbali ambayo si ya muhimu, kana kwamba wokovu huu unategemea juu ya mambo hayo. Kwa kufanya hivyo wanakiacha kitabu maalumu cha Mungu na kuwapa wanafunzi elimu pungufu na iliyo mbaya. 5 6T.150,151; Imepasa pawepo wanaume na wanawake ambao wamestahili kufanya kazi makanisani kuwafundisha vijana wetu kazi maalumu, kusudi watu wawezeshwe kumwona Yesu. Shule zilizowekwa nasi zapaswa ziwe na kusudi hili daima. Wala zisiige taratibu za shule za madhehebu zingine, au kufuata taratibu za vyuo vikuu (seminaries au colleges) vya kidunia. Wamepaswa wawe naKN 229.5

  utaratibu ulio bora zaidi ya shule zingine zote ambao hali ya ukafiri haiwezi kuonekana au kutokana nao ama kupendelewa nao. Wanafunzi hawana budi kufundishwa Ukristo wa kufaa, na Biblia imepasa ihesabiwe kuwa jambo kubwa kuliko mengine yote, na ya kwamba ni kitabu cha mafundisho kilicho cha maana sana. 6FE.231;KN 230.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents