Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwito Kusimama Imara

  Waadventista Wasabato hushughulika na maneno ya kweli yenye maana sana. Zamani zaidi ya miaka arobaini iliyopita (mwaka 1863), Bwana alitupa nuru ya pekee juu ya matengenezo ya afya, lakini tunaenenda jinsi gani katika nuru hiyo? Wangapi wamekataa kuyashika maonyo ya Mungu maishani mwao! Kama watu, yafaa tufanye maendeleo yanayolingana na nuru tuliyopokea. Ni wajibu wetu kufahamu na kuheshimu kanuni za matengenezo ya afya. Juu ya jambo hili la kuwa na kiasi yatupasa tuwashinde watu wote wengine; lakini hata hivyo wako miongoni mwetu washiriki wa kanisa waliofundishwa vizuri, hata wahubiri wa Injili, wasiojali ile kidogo tu, nuru ambayo Mungu ameitoa juu ya jambo hilo. Hula kama wapendavyo na kufanya kazi kama wapendavyo.KN 265.3

  Hebu wale walio walimu na viongozi kazini mwetu wasimame imara kuitetea Biblia juu ya matengenezo ya afya na kutoa ushuhuda wa dhati kwa wale wenye kusadiki kwamba tunaishi katika siku za mwisho wa historia ya dunia hii. Mstari wa kutofautisha baina ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wanaojitumikia wenyewe hauna budi kuchorwa.KN 265.4

  Nimeonyeshwa kuwa mafundisho tuliyopewa mwanzoni mwa ujumbe huu yangali na maana nayo yanapasa kuheshimiwa sana siku hizi kama yalivyokuwa yakiheshimiwa zamani. Kuna wengine umbao kamwe hawajaifuata nuru iliyokwisha kutolewa juu ya jambo hili la chakula. Sasa ndio wakati wa kuitwaa taa kutoka chini ya pishi na kuiacha iangaze vizuri, na kutoa nuru.KN 265.5

  Kanuni za afya zina maana sana kwa kila mmoja wetu na kwa sisi sote kwa jumla. Ujumbe wa matengeneo ya afya ulipoanza kunijia, nalikuwa dhaifu, mwenye kuzimia mara kwa mara. Nikamwomba Mungu msaada, naye akinifunulia jambo hili kuu la matengenezo ya afya. Akaniamuru kuwa wale wanaozishika amri zake hawana budi kutiwa kwenye umoja mtakatifu wake mwenyewe, na ya kwamba kwa kiasi katika kula na kunywa yawapasa kuitunza akili na mwili katika hali njema sana kwa kazi. Nuru hiyo imekuwa mbaraka mkubwa kwangu. Ninayo afya njema leo, ijapokuwa ninao umri mkubwa, kuliko niliokuwa nao siku za ujana wangu.KN 265.6

  Imesemekana kwamba sikuzifuata kanuni za matengenezo ya afya kama nilivyoziandika kwa kalamu yangu; lakini naweza kusema kuwa nimekuwa kiongozi mwaminifu wa matengenezo ya afya . Wale ambao wamekuwa watu wa nyumbani mwangu wanajua kuwa hilo ni kweli.KN 266.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents