Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Pata Upendo wa Mungu Maadam Unaweza

  Mawazo yangu hurudi nyuma kwa mwaminifu Ibrahimu, ambaye, kwa kuitii amri ya Mungu, alipewa katika njozi kule Beersheba, ashike nafasi yake akiwa pamoja na Isaka. Aliuona kwa mbele yake mlima ambao Mungu alikuwa amemwambia atamwonyesha kama mlima apaswao kutoa dhabihu juu yake.KN 208.1

  Isaka alifungwa kwa mikono itetemekayo, ya upendo wa baba yake mwenye huruma kwa sababu Mungu amemwamuru. Mwana huyo akakubali kutolewa dhabihu kwa sababu aliamini uaminifu wa baba yake. Lakini kila kitu kilipokwisha kuwa tayari, imani ya baba na utii wa mwana vilipokwisha kupimwa kabisa, malaika wa Mungu aliuzuia mkono wa Ibrahimu ulioinuliwa juu ambao ulikuwa karibu kumchinja mwanawe na kumwambia, yatosha. “Sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee” (Mwanzo 22:12).KN 208.2

  Tendo hili la imani kwa Ibrahimu limeandikwa kwa ajili ya faida yetu. Latufundisha fundisho kubwa la kuyatumaini masharti ya Mungu, ijapokuwa yawe mazito na makali namna gani; lawafundisha watoto utii kamili kwa wazazi wao na kwa Munga pia. Kwa utii wa Ibrahimu twafundishwa kwamba hakuna cho chote kilicho na thamani mno hata tusiweze kukitoa na kumpa Mungu.KN 208.3

  Mungu alimtoa Mwanawe kwa maisha duni, kujinyima, umaskini, taabu, shutuma, na kifo cha maumivu makubwa ya kusulibishwa. Lakini hapakuwako na malaika kutoa habari ya furaha: “Yatosha; huna haja ya kufa, Mwana mpendwa wangu.” Vikosi vya malaika vilikuwa vikingojea kwa huzuni, vikitumaini kuwa, kama ilivyokuwa kwa Isaka, Mungu katika dakika ya mvisho angezuia kifo chake cha aibu. Lakini malaika hawakuruhnsiwa kutoa ujumbe wo wote wa namna hiyo kwa Mwana mpendwa wa Mungu. Aibu katika jumba la baraza la hukumu na njiani kv.enda Fuvu la Kichwa ikaendelea, akaendelea, akadhihakiwa, akachekwa, na kutemewa mate. Akastahimili dhihaka, shutuma na matusi ya wale waliomchukia, mpaka juu ya msalaba akakiinamisha ki:hwa chake akafa.KN 208.4

  Mungu angeweza kutudhihirishia upendo wake kwa njia nyingine kuu kuliko hiyo ya kumtoa Mwanawe kupatwa na mateso hayo? Na kama karama ya Mungu kwa mwanadamu ilivyokuwa kipaji cha bure, na upendo wake usivyo na mwisho, kadhalika ndivyo madai yake juu ya matumaini yetu, utii wetu, moyo wetu wote, na wingi wa upendo wetu yasiyo na mwisho. Ahitaji yote awezayo mwanadamu kutoa. Utii wetu hauna budi kuwa wenye ulingamfu na kipawa cha Mungu; hauna budi kuwa kamili usiopungua cho chote. Wote tu wadeni wa Mungu. Anayo madai kwetu ambayo hatuwezi kuyatimiza pasipo kujitoa dhabibu kamili ya hiari. Adai utii wa upesi na wa hiari, wala hatakubali upungufu wo wote wa huo. Tunayo nafasi sasa kuupata upendo na kibali cha Mungu. Mwaka huu huenda ukawa mwaka wa mwisho wa maisha ya wengine walisomao neno hili. Kuna ye yote miongoni mwa vijana walisomao ombi hili ambaye angependa kuchagua anasa za ulimwengu huu badala ya ile amana ambayo Kristo humpa mwenye kuitafuta kwa moyo wa bidii na mwenye kufurahia kuyatenda mapenzi yake? 64T 630, 631;KN 209.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents