Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 27 - Mambo ya Fedha Nyumbani

  BWANA anapenda watu wake wawe wenye akili na uangalifu. Angependa wajifunze kuzuia upotevu wa fedha katika kila jambo, wasipoteze cho chote. Yawapasa kujua wakati wa kujiwekea akiba na wakati wa kutumia. Isipokuwa tunajikana nafsi na kuchukua msalaba, hatuwezi kuwa wafuasi wa Kristo. Tungepaswa kuona mambo yanayolazimu na kuyalipia malipo kamili kadin tuendeleavyo; iweni waangalifu wa mambo maaogo madogo; lipeni fedha mnayowiwa bila kukawia, na kujua kile kilicho halali yenu wenyewe. Yawapasa kuhesabu fedha ndogo ndogo zinazotumiwa tu kwa tamaa na kuongeza tamaa mbaya, na uteuzi wa chakula bure. Fedha inayotumiwa kwa vyakula vitamu visivyo na faida ingeweza kutumiwa kuongezea starehe na manufaa ya maana nyumbani mwenu. Si lazima kuwa bahili; yakupasa kuwa mwaminifu nafsini mwako na kwa ndugu zako. Ubahili ni jambo lisilo la haki kwa vipaji vya Mungu. Upotevu wa mali (Kuitapanya) ni vibaya pia. Fedha ndogo ndogo inayotoka ambayo wadhani haina maana kutaja huwa kitu kikubwa mwishowe.KN 175.1

  Unaposhawishiwa kutumia fedha kwa vitu vidogo vidogo vya mapambo, ungekumbuka kujikana nafsi na kujinyima jinsi ambavyo Kristo alistahimili ili awaokoe wanadamu walioanguka dhambini. Yawapasa watoto wetu kufundishwa kujinyima na kuitawala tamaa. Sababu ya watu wengi kuona kuwa wana shida katika mambo ni kwamba nawaziwekei masharti tamaa zao, tamaa za chakula na maelekeoyao. Kinachowafanya watu wengi kufilisika na kuiba mali ni kutamta kuzitimiza tamaa zipitazo kiasi za wake zao na watoto wao. Yawapasa akina baba na akina mama kuwa waangalifu kama nini kuwafundisha watoto wao uwekevu kwa maneno na kwa kielelezo pia!KN 175.2

  Si jambo zuri kujidai kuwa tajiri, au kuwa na hali yo yote ambayo kwa kweli hatuna-wafuasi wanyenyekevu wa Mwokozi mpole na mnyenyekevu wa moyo. Tusiudhike moyoni kama majirani zetu wakijenga na kutegemeza nyumba zao vizuri kwa njia tusiyoweza kufuata. Yambidi Yesu kutazama namna gani riziki za wale wenye kujipendeza nafsi wenyewe bila kujali wengine kwa tamaa ya chakula, kuwapendeza wageni wetu, ama kuridhisha tamaa zetu wenyewe bila kujizuia! Ni mtego kwetu kukusudia kufanya fahari au kuwaacha watoto wetu, waho chini ya mamlaka yetu, kufanya hivyo. 1AH7,19 - 384KN 175.3

  Cho chote kiwezacho kutumiwa kisitupwe. Kufanya hivi kunadai busara, na kufikiri kwanza, na uangalifu wa daima. Nimeonyeshwa kuwa kutoweza kujiwekea akiba, katika vitu vidogo vidogo, ni sababu ya jamaa wengi kuumia kwa kukosa riziki za maisha. 2CG 135;KN 175.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents