Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani Anatafuta Kudhoofisha Kujizuia

  Shetani hujitahidi kushusha kipimo cha usafi na hudhoofisha hali ya kujizuia ya wale wanaooana, kwa sababu ajua kuwa tamaa mbaya za mwili zikishinda, uwezo wa tabia ya adili utazidi kudhoofika, hivyo hana sababu za kujali maendeleo yao ya kukua kiroho. Pia ajua kwamba hawezi kwa njia yo yote nyingine, ila kwa njia hii tu, kutia vizuri chapa ya sanamu yake kwa watoto wao, na ya kuwa kwa njia hii aweza kuifanya tabia yao kuwa nyepesi kuliko awezavyo kufanya na tabia ya wazazi wao.KN 154.1

  Enyi wanaume na wanawake, siku moja mtafahamu tamaa ya mwili ilivyo na matokeo ya kuitimiza bila kujizuia. Ashiki mayostahili iliyo ya kawaida huweza kupatikana katika ndoa sawa na nje ya umoja huo. Matokeo ya kuzitimiza tamaa mbaya bila kujizuia ni nim? Chumba cha kulala, mahali ambapo malaika wa Mungu wangeongoza, hunajisiwa kwa mazoea haya mabaya. Na kwa sababu ya desturi mbaya za kinyama, zenye kuaibisha kabisa, miili imeharibiwa; mazoea ya kuchukiza mno huleta magonjwa mabaya. Kila ambacho Mungu alikitoa kiwe mbaraka kimefanywa kuwa laana.KN 154.2

  Kuzidi mno katika kutwaana kutaharibu upendo wa mazoea mema ya dini, kutanyang’anya ubongo nguvu zake zilizo faradhi kwa afya ya mwili na kutachosha kabisa nguvu za uhai. Haimpasi mwanamke awaye yote kumsaidia mumewe kwa kazi hii ya kujiangamiza mwenyewe. Hatafanya hivyo kama ameelimika na akiwa mwenye upendo wa kweli kwa mumewe.KN 154.3

  Kadiri tamaa mbaya za mwili zinavyotimizwa pasipo kujizuia, ndivyo zinavyozidi kuwa na nguvu, nazo zitazidi lcutaka zitimizwe. Hebu wanaume kwa wanawake wamchao Mungu wajue wajibu wao. Wengi wanaojidai kuwa Wakristo wana ugonjwa wa kupooza na ubongo kwa sababu ya kutokuwa na kiasi katika jambo hili.KN 154.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents