Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuitawala Tamaa ya Chakula na Uchu

  Mojawapo ya majaribu makali kabisa ambayo mtu hana budi kuyakabili ni juu ya jambo la tamaa ya chakula. Kuna uhusiano wa ajabu baina ya akili na mwili. Hugeuzana. Kuutunza mwili katika hali ya afya, kukuza nguvu zake, ili kila sehemu ya mashine hii yenye uhai ipate kutenda kazi vizuri, yafaa liwe jambo la kwanza kuangaliwa maishani mwetu. Kutoujali mwili ni kutozijali akili za moyoni. Mungu hawezi kutukuzwa watoto wake wakiwa wenye miili dhaifu, ama akili zilizodumaa. Kuiridhisha tamaa kwa kuihatarisha afya ni kuzitumia vibaya akili kwa jambo lisilo la haki, Wale wenye kushiriki namna yo yote ya kutokuwa na kiasi, katika kula ama katika kunywa, hutupa ovyo nguvu zao za mwili na kuudhoofisha uwezo wa tabia ya uadilifu. Wataona malipo ambayo hufuatana na uasi wa sheria za mwili. 273T 485, 486;KN 256.3

  Wengi hunyang’anywa nguvu za kazi akilini na mwilini pia kwa kula kupita kiasi na kujianisi. Tamaa za mwili hutiwa nguvu, huku hali takatifu na ya kiroho ikidhoofishwa. Tutakaposimama kukizunguka kile kiti kikuu cheupe cha enzi, habari za maisha ya wengi zitaonekana kuwa za ajabu kama nini. Ndipo wataona kile ambacho wangaliweza kufanya kama wasingaliuharibu uwezo wao waliopewa na Mungu. Kisha watatambua kipeo cha akili ambacho wangaliweza kupata kama wangalimpa Mungu nguvu zao zote za mwili na akili alizowakabidhi. Kwa majuto na maumivu mengi moyoni watatamani laiti wangeweza kuishi tena. 285T 135;KN 256.4

  Kila Mkristo wa kweli atatawala tamaa yake ya chakula pamoja na tamaa mbaya za mwili. Asipokuwa huru, na kutotawaliwa na tamaa ya chakula hawezi kuwa mtumishi mwaminifu na mtiifu wa Kristo. Kuiendekeza tamaa ya chakula na uchu ndilo jambo linalofanya ukweli usiwe na matokeo mema moyoni. Haiwezekani Roho na uwezo wa Neno la kweli kumtakasa mtu, roho, mwili na moyo, akiwa anatawaliwa na tamaa ya chakula pamoja na uchu. 293T 569, 570; KN 256.5

  Sababu kubwa iliyoacha Kristo astahimili kule kufunga muda mrefu jangwani ilikuwa kutufundisha jinsi ilivyo muhimu kujikana nafsi mwenyewe na kuwa na kiasi. Yafaa kazi hiyo ianze mezani mwetu nayo haina budi kufululizwa katika mambo yote yahusuyo maisha. Mkombozi wa ulimwengu alikuja kutoka mbinguni kusaidia mwanadamu katika udhaifu wake, ili, kwa uwezo ambao Yesu alikuja kumletea, apate kuwa mwenye nguvu kushinda tamaa ya chakula na uchu, na kuwa mshindaji wa kila jambo. 303T 488.KN 257.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents