Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kumkiri au Kumkana Kristo

    Katika kuchangamana kwetu na watu mtaani, jamaa, au katika uhusiano wo wote wa maisha tuwezapo kuwepo, ama kwa upungufu ama kwa wingi, kuna njia nyingi ambazo kwazo twaweza kumkiri Bwana wetu na njia nyingi ambazo kwazo kwa kusema mabaya juu ya wengine, kwa mazungumzo ya upuzi, ubishi na maneno ya mzaha, kwa maneno ya bure, yasiyo na maana, au maneno makali, ama kwa kusema uongo, kinyume cha kweli. Kwa maneno yetu twaweza kuonyesha kuwa Kristo hayumo ndani yetu. Kwa tabia yetu twaweza kumkana kwa kupenda raha, kwa kuepuka kazi na mizigo ya maisha ambayo mtu mwingine hana budi kuichukua kama sisi tusipoichukua, na kwa kupenda anasa za dhambi. Pia twaweza kumkana Kristo kwa kiburi cha anasa za dhambi. Pia twaweza kumkana Kristo kwa kupenda anasa za dhambi. Pia twaweza kumkana Kristo kwa kiburi cha nguo tuvaazo kwa kufuata mtindo wa walimwengu, au kwa mwenendo mbaya usio wa adabu. Twaweza kumkana kwa kuyapendelea maoni yetu wenyewe na kujaribu kuudumisha utu wa kale au kujihesabu wenyewe kuwa wenye haki. Pengine twaweza pia kumkana kwa kufikiri sana juu ya mambo mengi yadhaniwayo kuwa ni magumu na taabu kwetu.KN 94.1

    Hakuna mtu awezaye kumkiri Kristo kwa kweli mbele ya walimwengu isipokuwa nia na roho wa Kristo hukaa ndani yake. Haiwezekani kutoa kile tusicho nacho. Yapasa maongezi na mwenendo uonyeshe halisi na dhahiri neema na Kweli ya moyoni. Ikiwa moyo ni safi, mtiifu na mnyenyekevu, matunda yake yataonekana nje nayo yatakuwa kumkiri Kristo kwa nguvu kunakoleta kile kitakiwacho. 103T 331, 332.KN 94.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents