Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "undefined".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mvuto wa Masomo Mabaya Yasiyofaa

  Shetani anajua kuwa akili hupatwa sana na kile inachojilisha kwacho. Atafuta kuwaongoza vijana na wazee pia kusoma vitabu vya hadithi za uongo, na masomo mengine. Wasomaji wa vitabu vya jinsi hii huwa watu wasiofaa kwa kazi zilizowekwa mbele yao. Huishi maisha ya mashaka, na hawatamani kuyachunguza Maandiko Matakatifu, kujilisha Mana ya mbinguni. Akili inayohitaji kutiwa nguvu hudhoofishwa, na kupoteza uwezo wake wa kujifunza maneno makuu ya kweli yahusuyo utume na kazi ya Kristomaneno ya kweli ambayo yangeimarisha moyo, kuamsha akili, na kuchochea tamaa ya kushinda kama Kristo alivyoshinda.KN 191.3

  Kama ingaliwezekana sehemu kubwa ya vitabu vilivyokwisha kuchapishwa kutumiwa, baa linaloogofya sana watu akilini na moyoni lingezuiwa. Hadithi za mahaba, hadithi zisizo na maana zenye kusisimua, pia hadi vitabu vya jamii ile iitwayo hadithi za riwaya za kidini vitabu ambavyo ndani yake mwandishi hutia kwenye hadithi yake fundisho la wema na ubaya-ni laana kwa wasomaji. Maneno ya dini yaweza kuchanganywa katika kitabu cha riwaya, lakini-, mara nyingi Shetani hujivika mavazi ya malaika wema, apate kudanganya zaidi. Hakuna walioimarika katika mafundisno mazuri, wala hakuna wanaosalamika majaribuni, hata wasiweze kuwa hatarini kwa kujitoa kwa uovu unaoharibu hali ya kiroho, wenye kuliita giza uzuri wa Biblia. Huanzisha fadhaa, hutia wasiwasi akilini, hudnoofisha akili za moyoni zisiweze kuwa na manufaa, huiachisha roho ya mtu maombi, na kuiharamisha kwa ibada yoyote ya kiroho.KN 191.4

  Mungu amewajalia vijana wetu wengi kuwa wenye akili bora; lakini mara nyingi sana wamedhoofishwa uwezo wao, wakatatiza na kuziondolea akili zao nguvu kwa kiasi ya kwamba kwa muda wa miaka mingi hawajafanya maendeleo ya kukua katika neema au katika ufahamu wazi wa madhumuni ya imani yetu kwa ajili ya uchaguzi wao usio wa busara wa mambo wanayoyasoma. Wale wanaomtazamia Bwana kuja upesi, wenye kutazamia lile badiliko la ajabu, wakati ambapo “sharti huu uharibikao uvae kutokuharibiksa,” hawana budi wakati huu wa kuangaliwa kama twafaa au hatufai kusimama mahali pa juu zaidi katika kutenda mambo bora.KN 192.1

  Rafiki wapendwa, jiulizeni nafsi zenu wenyewe juu ya mvuto wa hadithi za kutahayarisha. Je, mnaweza, baada ya masomo ya jinsi hiyo, kuifungua Biblia na kuyasoma kwa moyo maneno ya uzima? Hamwoni kuwa Kitabu cha Mungu hakiwapendezi? Mvuto wa hadithi ya mahaba uko moyoni, ukiharibu hali njema ya moyoni, na kukufanya usiweze kukaza fikra zako juu ya maneno makubwa na mazito ya kweli yenye kuihusu hali yako ya milele.KN 192.2

  Kwa moyo thabiti kataa masomo yote ya ovyo. Hayatakutia nguvu rohoni mwako, bali yataingiza akilini mambo ambayo yatapotosha mawazo, na kukufanya umdharau Yesu na kutokuyafikiri sana mafundisho yake yenye thamani. Jiepushe moyoni na mambo yote ambayo yaweza kuipotosha akili. Usiichoshe kwa hadithi hafifu zisizotia nguvu akilini. Mafikara huwa ya namna ile ile ya chakula ambacho ubongo hulishwa kwacho. 2 MYP 271 - 273;KN 192.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents