Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kusoma Biblia Huzitia Akili Nguvu

  Kama Biblia ingesomwa kama ipasavyo, watu wangekuwa wenye nguvu akilini. Mafundisho yaliyoelezwa katika Neno la Mungu, urahisi wao mkuu, mambo bora ambayo Neno la Mungu huyatia akilini hukuza uelekevu ndani ya mtu ambao bila ya hayo usingekuzwa. Katika Biblia kuna nafasi kubwa isiyo na kikomo ya akili. Mwanafunzi wa Biblia atatoka katika kuyatafakari mambo makuu ya Biblia akiwa safi zaidi, hali ameadilishwa mawazoni na kuwa na furaha moyoni kuliko kama angeutumia wakati huo kusoma kitabu cho chote kingine kilichotungwa na mwanadamu, hasa neno lo lote la hizo zenye tabia hafifu. Akili za vijana hukosa kuyafikia maendeleo yao bora kabisa wanapokataa chimbuko bora sana la hekima-Neno la Mungu. Kisa kinachoacha tuwe na watu wachache tu wenye nia njema, imara na thabiti ni kwa kuwa Mungu haogopwi, Mungu hapendwi, kanuni za dini hazifuatwi maishani kama lpasavyo. Mungu angependa tufaidi kila njia ya kukuza naKN 102.5

  kuimansha uwezo wa akili zetu Kama Biblia ingesomwa zaidi, kama maneno yake ya kweli yangefahamika vizuri, tungekuwa watu wenye hekima na zaidi. Nguvu hutiwa moyoni mwa mtu kwa kuzichunguza kurasa zake. 12CG 507;KN 103.1

  Mafundisho ya Biblia yana maana kubwa juu ya mafanikio ya mtu kuhusu mambo yote ya miasha haya. Huzifunua kanuni ambazo ni jiwe kuu la pembeni la mafanikio ya taifa-kanuni ambazo kwazo hufungwa hali njema ya maisha ya watu kwa jumla, na ambazo ni kitu kinacholinda usalama wa watu nyumbanikanuni ambazo pasipo kuwa nazo mtu hawezi kupata manufaa, furaha, wala heshima katika maisha haya, wala hawezi kutumaini kuupata uzima wa milele wa siku zijazo. Hakuna mahali maishani, ama namna ya mambo yampatayo mwanadamu maishani mwake, ambapo mafundisho ya Biblia hayamtayarishi mtu na kumsaidia katika hali hizo. 13PP 599;KN 103.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents