Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Umoja na Kristo na Umoja Baina Yetu Ndio Usalama Wetu

    Walimwengu wanapendezwa kuona mafarakano miongoni mwa Wakristo. Wasioamini wanapendezwa sana. Mungu anahitaji watu wake wabadilike. Umoja na Kristo na umoja baina yetu ndio usalama wetu siku hizi za mwisho. Tusimpe nafasi shetani kuwasonda vidole washiriki wetu wa kanisa, akisema: “Tazama jinsi watu hawa, wasimamao chini ya bendera ya Kristo, wanavyochukiana. Hatuna sababu ya kuwaogopa wakiwa wanatumia nguvu nyingi zaidi kugombana wao kwa wao kuliko wanayoitumia vitani kupigana na majeshi yangu.”KN 49.2

    Baada ya kushuka kwa Roho Mtakatifu wanafunzi walitawanyika kuhubiri habari za Mwokozi aliyefufuka, shauku yao ilikuwa moja tu, wokovu wa roho za watu. Walifurahia utamu wa ushirika wa watakatifu. Walikuwa wenye upendo, waangalifu, wenye kujikana nafsi, walio tayari kujinyima cho chote kwa ajili ya kweli. Katika kushirikiana wao kwa wao kila siku waliudhihirisha upendo ambao Kristo alikuwa amewaamuru kuuonyesha. Kwa maneno ya ukarimu, na matendo mema walijitahidi kuwasha upendo huu mioyoni mwa wengine.KN 49.3

    Waumini walipaswa daima kuufurahia upendo uliojaza mioyo ya mitume baada ya kushukiwa na Roho Mtakatifu. Walipaswa kusonga mbele kwa utii wa hiari ya moyo kwa ile amri mpya: “Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” (Yohana 13:34). Hivyo walipaswa kuungwa katika umoja na Kristo ili wapate kuwezeshwa kuyatimiza matakwa yake. Uwezo wa Mwokozi ambaye angeweza kuwahesabia haki kwa haki yake ulikuwa hauna budi kukuzwa.KN 50.1

    Lakini wale Wakristo wa kwanza wakaanza kutafutana makosa. Kwa kutumia muda wao katika kukosoana, kutoa nafasi kwa lawama zisizo na huruma, wakashindwa kumwona Mwokozi na upendo mkuu aliokuwa amewafunulia wenye dhambi. Wakawa wakali zaidi kwa habari za kawaida za matendo ya dini ya nje, hasa juu ya kanuni za imani, wakazidi sana kuwa wakali katika ukosoaji wao. Katika jitihada zao kuwahukumu wengine wakasahau makosa yao wenyewe. Wakasahau fundisho la upendo wa kindugu ambalo Kristo alikuwa amewafundisha. Na jambo la kusikitisha kuliko yote, walikuwa hawafahamu upotevu wao. Hawakujua kwamba furaha na raha zilikuwa zikiondoka maishani mwao, na ya kuwa punde wangetembea gizani, wakiwa wameufungia upendo wa Mungu nje ya mioyoni mwao.KN 50.2

    Mtume Yohana alifahamu kuwa upendo wa kindugu ulikuwa ukipungua kanisani, naye alikazia hasa juu ya jambo hili. Mpaka siku ya kufa kwake aliwasihi waumini kuonyesha daima kupendana wao kwa wao. Nyaraka zake kwa makanisa zinajaa wazo hili. Ameandika, “Wapenzi, na tupendane; kwa kuwa pendo ni la Mungu Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni ili tupate uzima kwa yeye Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana” (1 Yohana 4:7-11).KN 50.3

    Katika kanisa la Mungu siku hizi upendo wa kindugu unakosekana sana. Wengi wa wale wanaodai kuwa wanampenda Mwokozi hawawapendi wale ambao wanaungana nao katika ushirika wa Kikristo. Tu watu wa dini moja, watu wa nyumba moja, wote watoto wa Baba, yule yule mmoja wa mbinguni, wenye tumaini lile lile la baraka la kutokufa. Basi kifungo kinachotufunga pamoja kingekuwa imara na cha upendo kama nini! Walimwengu wanatutazama kuona kama imani yetu inatoa mvuto unaotakasa juu ya mioyo yetu. Ni wepesi kuona kila kosa katika mienendo yetu, kutokupatana ko kote katika matendo yetu. Hebu tusiwape nafasi kuilaumu dini yetu. 28T 240-242;KN 50.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents