Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jibu la Mkristo kwa Mtu Asiyeamini

    Kila Mkristo apaswa kufanya nini akiingizwa mahali pa kujaribiwa nguvu ya imani yake? Kwa uthabiti wenye kustahili kuigizwa yampasa aseme dhahiri: “Mimi ni Mkristo mwaminifu. Naamini kuwa siku ya saba ya juma ni Sabato ya Biblia. Imani na kanuni zetu zimeachana, ni tofauti hata hazipatani. Hatuwezi kufurahi pamoja, maana kama nikiendelea kujipatia ujuzi kamili zaidi wa mapenzi ya Mungu, nitazidi kuhitilafiana na walimwengu na kufanywa nifanane zaidi na Kristo. Kama ukiendelea kutoona uzuri ndani ya Kristo, wala mivuto katika Neno la kweli, utapenda ulimwengu, ambao mimi siwezi kuupenda, nikiwa nayapenda mambo ya Mungu, usiyoweza kuyapenda. Mambo ya kirono hufahamika kiroho. Pasipo ufahamu wa Kiroho hutaweza kuyaona madai ya Mungu kwangu, ama kujua wajibu unaonipasa kwa Bwana ninayemtumikia; kwa hiyo, utaona kwamba sikujali kwa ajili ya wajiou wa dini. Hutafurahi; utakuwa na wivu kwa sababu ya upendo ambao ninamtolea Mungu, nami nitakuwa hali ya upweke katika imani yangu ya dini. Maoni yako yatakapogeuka, moyo wako utakapoitikia madai ya Mungu, nawe utakapojifunza kumpenda Mwokozi wangu, ndipo uchumba wetu utakapoweza kufanywa upya.”KN 142.1

    Hivi ndivyo mwenye kuamini anavyojinyima kwa ajili ya Kristo na kujitoa dhabihu ambayo huipendeza dhamiri ya moyoni mwake, na yenye kuonyesha kwamba nuuthamini uzima wa milele hata kukaa bila kuolewa kuliko kuungamanisha moyo wake wa kuupenda uzima na mtu mwenye kupendeleza anasa za dunia badala ya kumpenda Yesu, na ambaye angependa kumpotosha auache msalaba wa Kristo.KN 142.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents