Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  “Ninyi si Mali Yenu Wenyewe”

  Twaamini bila mashaka kuwa Kristo yu karibu kuja. Hii si hadithi tu kwetu; ni jambo la hakika. Ajapo natapaswa kutusafisha dhambi zetu, kutuondolea makosa katika tabia zetu, wala kutuponya udhaifu wa hali ya moyo na tabia zetu. Ikiwa haina budi kutendwa kwa ajili yetu, kazi hiyo yote yapasa kutekelezwa kabla ya wakati huo.KN 243.1

  Bwana ajapo wale walio watakatifu watazidi kutakaswa. Wale ambao wamehifadhi miili na roho zao katika utakatifu, katika usafi na kicho, ndipo watapokea mguso wa mwisho wa kutokufa. Lakini wale wasio na haki, wasiotakaswa, na wachafu watadumu hali hiyo milele. Basi, hakuna kazi watakayotendewa kuondoa makosa yao na kuwapa tabia takatifu. Hiyo yote haina budi kutendwa saa hizi za kuangaliwa kama twafaa au hatufai. Sasa ndio wakati upasao kazi hiyo kutekelezwa kwetu.KN 243.2

  Tumo katika ulimwengu ambao umezuiwa usipate haki na usafi wa tabia, pamoja na kukua katika neema. Po pote tunapotazama twaona uchafu na unajisi, ubaya na dhambi. Basi, ni kazi gani tupaswayo kujaribu kuifanya hapa kabla hatujaupokea uzima wa milele? Ni kuiweka miili yetu katika hali takatifu, roho zetu katika hali safi, ili tupate kusimama pasipo mawaa katikati ya makosa yanayojaa pande zote kutuzunguka siku hizi za mwisho.KN 243.3

  Hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu” (1 Wakorintho 6:19, 20).KN 243.4

  Sisi si mali yetu wenyewe. Tumenunuliwa kwa gharama ya thamani kubwa, naam, mateso na mauti ya Mwana wa Mungu. Ikiwa tungelifahamu neno hili, na kulitambua kabisa, tungeona moyoni kuwa wajibu mkuu unatukalia kujitunza katika hali bora kabisa ya afya, ili tupate kumtumikia Mungu kwa ukamilifu. Lakini, tukifuata njia ambayo hutumia nguvu zetu za uhai, na kupunguza nguvu zetu, au kutia giza akilini, twatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa kufuata njia hiyo hatumtukuzi katika miili wala katika roho zetu ambazo ni mali yake, bali tunafanya kosa kubwa machoni pake. 32T 354 - 356; KN 243.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents