Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    28 — Mathayo: Kutoka Kutoza Ushuru Mpaka Mwanafunzi

    Wakuu wa Kirumi katika Palestina walikuwa wamechukiwa sana. Na kwa kuwa kodi ilitozwa na watawala wa kigeni, lilikuwa chukizo la daima, linalowakumbusha kuwa kujitawala kwao kumekoma. Watoza kodi hawakuwa vyombo vya Warumi tu, bali walikuwa wenye uchu wa kujitajirisha kwa njia ya kidhalimu, na kuwatoza watu isivyo haki. Myahudi aliyefanya kazi hii alidharauliwa sana na kutiwa katika fungu la watu waovu.TVV 147.1

    Lawi Mathayo alikuwa wa namna hii, ambaye aliitwa kufanya kazi ya Kristo. Mathayo alikuwa amesikia mahubiri ya Kristo, na kwa kadiri Roho wa Mungu alivyomdhihirishia dhambi zake alitamani kwenda kwa Kristo, ili apate msaada, lakini alivyokuwa amezoea kutengwa na Marabi, na kuhesabiwa kuwa mtu mwovu hakuwa na atumaini kuwa Mwalimu Mkuu huyu angemjali.TVV 147.2

    Siku moja akiwa ameketi katika chumba chake cha kutozea kodi, mtoza ushuru huyu alimwona Yesu akitokea. Alishangaa mno aliposikia maneno yakimwambia, “Nifuate”.TVV 147.3

    Mathayo “akaacha vyote, akainuka, akamfuata.” Mathayo hakukawia, wala hakuuliza swali lolote kuhusu kazi au mali au ufukara wake kama akifuata kazi hiyo. Ilimtosheleza kuwa pamoja na Yesu, ili aweze kusikiliza maneno yake, na kushirikiana naye katika kazi yake.TVV 147.4

    Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika wakati Yesu alipowaita akina Petro na wenzake, ili wamfuate. Waliacha mashua zao na nyavu zao mara moja wakamfuata. Wengine walikuwa na watu waliowategemea ili wawape mahitaji yao, lakini walipokubali mwaliko wa Mwokozi, hawakuuliza kuwa, “Tutaishije na kusaidia watu wanaotutegemea?” Baadaye Yesu alipowauliza: “Je, hapo nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu, mlipungukiwa na kitu? Wakasema.” Luka 22:35.TVV 147.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents