Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    “Mtindo Mpya” wa Uongo wa Shetani

    Kuwa sehemu fulani ya sheria iliyotamkwa na sauti ya Mungu mwenyewe imewekwa kando ndilo dai ambalo Shetani sasa hujitahidi kulitoa. Haihitaji kuishambulia sheria yote; ikiwa anaweza kuwaongoza wanadamu kutoijali kanuni moja, kusudi lake hutimia. Kwa “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akijikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.” Yakobo 2:10. Kule kukubali kuvunja amri moja wanadamu huwa mateka chini ya mamlaka ya Shetani. Unabii huonya juu ya ile nguvu kuu ya uasi, itendayo kazi kwa niaba ya Shetani. “Naye atanena maneno kinyume chake Akaye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mkononi mwake.” Daniel 7:25. Watu wataweka sheria zao kutenda kazi kinyume cha sheria ya Mungu, na katika juhudi zao kulazimisha utii kwa sheria hizi watawatesa wanadamu wenzao.TVV 433.5

    Vita dhidi ya sheria za Mungu itaendelea mpaka mwisho wa dunia. Watu wote watatakiwa wachague baina ya sheria za Mungu na zile za wanadamu. Kutakuwa na makundi mawili tu. Kila tabia itadhihirika kikamilifu. Wote wataonyesha ikiwa wamechagua kuwa watii au kuwa waasi.TVV 434.1

    Kisha mwisho utakuja. Mungu ataidhibitisha sheria yake, na kuwaokoa watu wake. Shetani na wale wote wanaomuunga mkono katika uasi watakatiliwa mbali. Dhambi na wenye dhambi vitaangamizwa, shina na tawi.” (Tazama Malaki 4:1.) Hili silo tendo dhalimu kwa upande wa Mungu. Wakataaji Wa rehema zake wanavuna walichopanda. Mungu ni chemichemi ya uzima, na mtu akichagua dhambi, hujiondoa mwenyewe kutoka uzima. Kristo anasema, “Na wao wanichukiao hupenda mauti.” Mithali 8:36. Mungu huwapa maisha ili wapate kukuza tabia yao na kudhihirisha kanuni zao. Hii ikikamilika, watapokea thawabu ya uchaguzi wao wenyewe. Shetani na wale wote wanaojiunga naye hujikinga kando na amani ya Mungu kiasi kwamba kuwako kwake Aliye upendo kutawaangamiza.TVV 434.2

    Mwanzo wa pambano kuu, malaika hawakulielewa vema. Kama Shetani na wafuasi wake wangaliangamizwa papo hapo, mashaka kuhusu wema wa Mungu yangalibaki mawazoni mwao na hivyo kuwa mbegu mbaya ambayo ingezaa tunda lake la dhambi ya mauti.TVV 434.3

    Lakini haitakuwa hivyo baada ya pambano kuu kumalizika. Hapo mpango wa Mungu wa ukombozi ukiwa umekamilika, tabia ya Mungu imedhihirika kwa viumbe wote. Kanuni za sheria yake zinaonekana kuwa kamilifu na zisizobadilika. Dhambi imedhihirisha asili yake, Shetani tabia yake. Kuangamizwa kwa dhambi kutathibitisha upendo wa Mungu na kuanzisha heshima yake mbele za ulimwengu wote.TVV 434.4

    Hapo basi, huenda malaika wakafurahia kumtazama Mwokozi akiwa msalabani; kwa sababu hata kama hapo mwanzo hawakuelewa yote, walifahamu kuwa kuangamizwa kwa Shetani kulihakikishwa, ukombozi wa mwanadamu hakika, na ulimwengu kufanywa salama milele.TVV 435.1

    Kristo Mwenyewe alitambua matokeo ya kafara iliyofanywa Kalwari. Aliyatazamia haya yote alipolia kwa sauti ya kushangilia akiwa msalabani na kusema, “Imekwisha.”TVV 435.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents