Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ondoa Giza kwa kuruhusu Nuru

    Yesu hakuwakanusha wapinzani wa dini, waliokuwa wanatafuta nafasi ya kumshambulia. Lakini kwa njia ya kisa kidogo rahisi aliwapa kitu kilichowaeleza upendo wa kimbingu ulivyo. Kisa hicho kilitosheleza, hata yule mwanasheria akaungama. Njia bora ya kushughulikia makosa ni kueleza ukweli ulivyo. Yesu akasema: “Kulikuwa na mtu aliyekuwa akisafiri toka Yerusalemu kwenda Yeriko. Akaangukia katika kundi la maharamia, waliomnyang’anya mali yake, na kumpiga sana, wakamwacha nusu ya kufa. Kwa bahati Kuhani alikuwa akienda katika njia hiyo hiyo, alipomwona, akapitia kando upande mwingine akaenda zake. Hali kadhalika na Mlawi pia akapita, alipomwona akapita upande. Mfano huu haukuwa jambo la kubuni, ila lilitokea hakika. Kuhani na Mlawi walikuwako katika kundi lililokuwa likimsikiliza.TVV 282.1

    Njia ya kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko ilikuwa ikipitia katika msitu wa mawe mawe uliokuwa ukikaliwa na maharamia. Kila mara mahali hapo palikuwa penye matendo ya ujangili. Hapo ndipo yule msafiri aliposhambuliwa, akaachwa nusura kufa. Kuhani alimtazama tu akapita upande. Mlawi alijisikia kuwa anapaswa kumsaidia, lakini aliona kuwa jambo hilo halimhusu. Watu hawa wote walikuwa wateule waliopaswa kutenda mambo kama hayo. Wote walitazamiwa na watu kuwa ni wajumbe wanaoaminiwa, kuwaonea huruma walio kando ya njia. Waebrania 5:2.TVV 282.2

    Malaika wa mbinguni huangalia kwa wenye dhiki walioko duniani, nao huwa tayari kushirikiana na wanadamu ili kuwasaidia. Mbinguni hutazama kama Kuhani na Mlawi watawahurumia wenye dhiki na shida. Mwokozi alikuwa amewafundisha Waebrania jangwani mafundisho yote muhimu kuhusu mahitaji ya wanadamu na mambo yote ambayo watu wangalipata kwa makuhani na walimu wao. Ujumbe kamili ulitolewa kwa Musa na Bwana Mungu kwamba wawaangalie wasiokuwa na wazazi na maskini, na wageni “wapendeni basi wageni.” “Mtawapenda kama nafsi zenu.” Torati 10:18, 19; Mambo ya Walawi 19:34.TVV 282.3

    Lakini watu hao walifundishwa katika skuli za kidini ya taifa ambayo ni ya ushindani, Kuhani na Mlawi wamekuwa wenye ubinafsi, watu wenye mawazo hafifu sana wenye kujipenda kama si watu wa dini. Wakati walipomwangalia yule mtu aliyejeruhiwa hawakuweza kutambua kama ni mtu wa kwao au mwingine. Walidhani ya kuwa ni Msamaria tu wakageukia mbali.TVV 282.4

    Sasa akaja Msamaria akamwona yule aliyejeruhiwa akamhurumia. Msamaria alijua wazi kwamba, hali yao ya kubezwa na Wayahudi, wasingalifadhiliwa, wangalipitwa tu. Yeye pia aliliofia hali yake asije akawa hatarini kwa kukawia mahali hapo. Ilitosha kuwa, yupo binadamu anayehitaji msaada. Alitwaa vazi lake na kumfunika. Mafuta ya divai alivyochukua kwa safari yake alivitumia kumgangia. Alimpandisha juu ya mnyama wake, akamchukua taratibu akampeleka mpaka nyumba ya wageni apate kulala hapo na kutunzwa.TVV 283.1

    Asubuhi yake Msamaria, kabla ya kwenda zake alimkabidhi katika mikono ya mwenye nyumba, baada ya kulipa gharama, na kutoa fedha za zaidi kwa ajili ya kumtunza, akaenda zake. Akatoa na ahadi kuwa kama akigharimiwa zaidi, arudipo, atalipa.TVV 283.2

    Habari ikaishia hapo. Yesu akamkazia mwanasheria macho, akasema, “Katika watu hawa watatu, ni nani aliyekuwa jirani yake?” Mwanasheria akajibu, ‘Ni yule aliyemhurumia.” Yesu akasema: “Nenda ukafanye mambo kama hayo.”TVV 283.3

    Swali kwamba “Jirani yangu ni nani”, lilijibiwa kabisa. Jirani zetu ni kila binadamu anayehitaji msaada wetu. Kila mtu aliyejeruhiwa na kuumizwa na mwovu Shetani, kila aliye mali ya Mungu ni jirani yangu.TVV 283.4

    Katika kisa cha Msamaria mwema, Yesu alieleza mambo yanayomhusu Yeye na kazi yake. Mtu alikuwa amejeruhiwa na kuumizwa na kuachwa nusura ya kufa, ameachwa katika mikono ya Shetani. Lakini Mwokozi aliacha fahari yake na utukufu wake akaja kutuokoa. Aliponya majeraha yetu, akatufunika na vazi lake la haki. Alitoa gharama yetu yote kabisa. Akieleza kielelezo chake, aliwaambia wasikizi wake: “Kama nilivyowapenda ninyi . . . mpendane vivyo hivyo.” Yohana 13:34.TVV 283.5

    Msamaria alitii na kufuata kanuni ya wema na upendo wa moyoni, na kwa jinsi hii alijionyesha kuwa yeye ni mtendaji wa sheria. Kristo alimwagiza mwana sheria akisema: “Enenda ukatende hivyo.”TVV 283.6

    Fundisho hilo si kama halitakiwi leo. Ubinafsi na hali ya ubaridi maishani imezimisha moto wa upendo katika maisha ya wakristo, na kuondoa hali ya uchangamfu katika tabia ya wengi. Watu wanaolitaja jina lake wamesahau kuwa ukristo ni kufanana na Kristo mwenyewe. Isipokuwa maisha yetu yamfuatishe Kristo popote tulipo, hata kama tuwe na cheo gani kanisani, hatuwi watu wa Kristo.TVV 283.7

    Kristo atuambia tuwe kama yeye katika kuwahudumia watu. “Mmepata bure, toeni bure.” Mathayo 10:8. Huo ndio usemi wa Kristo. Wengi hushindwa na kuona aibu na upotevu katika hali yao mbaya. Wanaishi kwa njaa na kiu. Watu kama hawa wanahitaji huduma halisi kwa wakristo. Huangalia makosa yao mpaka wakakata tamaa. Kama sisi ni wakristo, tuwaonapo wanadamu kwa hali hiyo, kwamba ni katika dhiki au, katika dhambi, tusiseme kuwa, mambo hayo hayanihusu.TVV 284.1

    Habari ya Msamaria mwema, na tabia ya Kristo, hudhihirisha maana ya sheria na kutenda kwake, jinsi isemavyo kumpenda jirani kama nafsi yako. Wakati wana wa Mungu wakidhihirisha tabia hiyo kwa watu wote, huwa mashahidi kamili wa sheria ya mbinguni. “Tukipendana Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake hukamilika kwetu.” 1 Yohana 4:12.TVV 284.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents