Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Waongon wa Dini waliwapotosha watu wengi kumkataa Kristo

  Yesu alisema: “Nawaambieni itakuwa heri kwa Sodoma siku ile kuliko mji ule.” Halafu mawazo yake yaligeukia miji ya Galilaya ambako amefanya kazi nyingi zaidi. Kila siku Mkuu wa uzima alikuwa akiingia na kutoka katika miji hiyo. Utukufu wa Mungu umekuwa ukiangaza kwao na walikuwa wakimfuata Mwokozi hatua kwa hatua. Hata hivyo wameukataa ujumbe wa kipawa cha mbinguni. Marabi walikuwa wamewaonya watu wasije kupokea mafundisho ya mwalimu mpya huyu. Badala ya kulipata neno la Mungu na kujisomea wenyewe, watu walifuata tu mambo waliyoelekezwa na makuhani na waongozi wa dini, na kumkataa mkuu wa uzima na ukweli anaoufundisha. Wakachagua kufuata mapokeo na kukataa kweli. Wengi walikuwa kama waongofu, lakini hawakushika kamili njia ya uongofu halisi. Kwa hiyo waliukataa ukweli ambao ungewaletea wokovu.TVV 277.4

  Shahidi wa kweli husema: “Tazama nasimama mlangoni, nabisha.” Ufu. 3:20. Kila neno la kuingilia katika uongofu lisemwalo na wajumbe wa Mungu ni mbisho katika mlango wa moyo wa mtu. Ni sauti ya Yesu akibisha ili afunguliwe. Kila kubisha kusikoitikiwa, humfanya mtu kuwa mgumu zaidi na zaidi. Moyo huzoea ufedhuli na kutojali. Hukumu ya Mungu haitakuja kwa sababu tumekuwa tukiishi katika makosa, ila kwa sababu tumekataa kujali njia za Mungu za kutusaidia tuifikie kweli.TVV 278.1

  Kazi yao ilipomalizika, wale sabini walirudi kwa furaha wakisema: “Nilimwona Shetani kama umeme akianguka kutoka mbinguni.” Yesu alitazama kupita kwenye msalaba wa Kalwari na mateso yake na aibu akaona shindano kuu la mwisho, wakati Shetani atakapoangamizwa ndani ya dunia iliyokuwa imechafuliwa vibaya na udanganyifu wake, na uasi.TVV 278.2

  Tangu hapo wafuasi wa Yesu lazima wamwangalie Shetani kama adui ambaye ameshindwa tayari. Katika msalaba alipata ushindi kwa ajili ya wafuasi wake. Ushindi huo ndio Kristo anawatakia wafuasi wake wote,waupate uwe wao. Asema, “Tazama, nimewapa uwezo wa kuwakanyaga nyoka, na nge, na nguvu zote za yule mwovu, wala hakuna kitu kitakachowashinda.” Nguvu za Mwenyezi na Roho Mtakatifu ni ngome ya kila mfuasi wa kweli wa Kristo. Hakuna mfuasi wa kweli mwenye kutubu kikweli anayedai ulinzi kwa Kristo, atakayepitwa tu na kuachwa katika uwezo wa mwovu Shetani. Majaribu na matatizo yanapokuja, tumtazame Yesu, ambaye ndiye msaada wetu. Tumshukuru Mungu, kwa kuwa tunaye Mwokozi hodari, aliyemfukuza mwovu kutoka mbinguni. Kwa nini tusizungumze juu yake na ushindi wake? Mungu hatawaacha kamwe watu wake washindane wenyewe na yule mwovu Shetani.TVV 278.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents