Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  34 — Nira Yake ni Laini na Mzigo Wake ni Mwepesi

  “Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Mwokozi hakumwacha mtu yeyote nje bila kumshughulikia, kwa upendo na uangalizi. Huwaangalia wenye dhiki na wenye wasiwasi, watu ambao hawana matumaini yoyote, wala utulivu katika mioyo yao, naye huwaalika wamjie ili wapate pumziko kwake.TVV 179.1

  Huwaambia wenye kusumbuka kwamba: “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu, maana mimi ni mpole, na mnyenyekevu wa moyo, nanyi mtapata pumziko mioyoni mwenu.”TVV 179.2

  Kwa maneno haya Kristo huwazungumzia watu wote wenye kujua na wasiojua pia, wote wenye kulemewa na mizigo, ambayo ni Kristo peke yake awezaye kuwatua. Mizigo mizito zaidi ni ile ya dhambi. Kama tukiachwa kuichukua sisi wenyewe, itatukandamiza na kutuseta na kutupondaponda. Lakini Kristo ambaye hana dhambi ametuchukulia. “Bwana ametwika maovu yetu sisi sote.” Isaya 53:6. Amechukua mizigo ya maovu yetu. Mizigo ya masikitiko yetu na maafa yetu pia amechukua.TVV 179.3

  Ndugu mkubwa wa jamaa yetu huishi milele katika kiti chake cha enzi. Anajua kabisa udhaifu wa wanadamu, maana aliupitia; mahitaji yetu, na haja zetu zote. Pia anajua uwezo wa majaribu, maana alijaribiwa katika mambo yote bila kutenda dhambi. Je, unajaribiwa? Atakuokoa. je, wewe ni dhaifu? Atakutia nguvu. Je, wewe hujui lolote? Atakuelimisha. Je, una majeraha? Atakuponya. “Atawaponya waliovunjika mioyo, na kuwaganga wenye majeraha.” Zaburi 147:3.TVV 179.4

  Kwamba matatizo yako ni makubwa kadiri gani, mwambie Bwana. Roho yako itatakasika kiasi cha kudumu. Njia itafunguliwa kwako kwa matatizo na matisho yote. Mzigo wako mzito utakuwa mwepesi zaidi wa kufurahisha. Pumziko Kristo ambalo hutolewa na Yesu, lina masharti, lakini limetajwa dhahiri. Wote waweza kulipata.TVV 179.5

  “Jitieni nira yangu.” Nira ni kitu cha huduma. Ng ombe hutiwa nira ili kutumika na ili watumike kwa urahisi na ufanisi. Kwa kielelezo hicho Yesu hufundisha kuwa tumeitwa kwa utumishi. Kwa hiyo tunapaswa kuchukua nira yake.TVV 180.1

  Nira hiyo ni sheria za Mungu, ambazo zimeandikwa ndani ya mioyo. Humwunganisha mtenda kazi wa Mungu na mapenzi ya Mungu. Kama tungaliachwa kuenenda jinsi tupendavyo, tungelitumbukia katika mashimo ya Shetani. Kwa hiyo Mungu hutufunga katika mapenzi yake.TVV 180.2

  Nira ya kazi Kristo amekwisha kuichukua badala ya wanadamu. Alisema, “Nalishuka kutoka mbinguni siyo kufanya mapenzi yangu, ila kufanya mapenzi yake aliyenipeleka.” Yoh. 6:38. Upendo kwa Mungu, juhudi kufanya mapenzi yake, na utukufu wake, na upendo kwa wanadamu waliopotea, ndivyo vilimleta Yesu duniani. Jambo hili ndilo lilikuwa likimlazimisha, katika maisha yake yote hapa duniani. Kanuni hii alituachia pia tuwe nayo.TVV 180.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents