Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mzunguko wa Mavuno ya Injili

    “Avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda katika uzima wa milele, ili wote, yeye apandaye naye avunaye wafurahi pamoja.” Huu ni usemi wa kweli kwamba mmoja hupanda na mwingine huvuna. Wale wanaopokea Injili huwa wajumbe wake walio hai. Mmoja hupanda mbegu; mwingine hukusanya mavuno; wote hufurahia pamoja thawabu ambayo ni malipo ya kazi.TVV 101.6

    Yesu alisema kwa wanafunzi wake. “Niliwatuma ninyi mkavune pale ambapo hamkupashughulikia. Watu wengine walipashughulikia, na ninyi mkaingia katika kazi yao. Wanafunzi walikuwa wanaingia katika kazi za watu wengine. Mjumbe asiyeonekana alifanya kazi kimya kimya, lakini mavuno yalipatikana. Kristo alikuwa karibu kuzimwagilia mbegu kwa damu yake mwenyewe. Wanafunzi walikuwa wenzake Kristo katika kazi pamoja na watakatifu wa zamani. Kwa njia ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, watu maelfu waliongolewa kwa siku moja. Hii ilkuwa kazi ya kupanda ya Kristo, na mavuno ni ya kazi yake.TVV 101.7

    Wasamaria walikuja wakamsikiliza Yesu, wakaamini. Kundi kubwa la watu waliomzunguka kisimani, walimsikiliza kwa makini, na kuuliza mambo mengi ambayo hayakujulikana kwao zamani. Mashaka ya kila namna waliyokuwa nayo yalianza kutoweka. Wakitamani kumsikiliza zaidi, wakamkaribisha katika mji wao kwa muda wa siku mbili alikaa na Wasamaria hao, na matokeo yalikuwa makubwa, maana watu wengi waliamini.TVV 102.1

    Yesu hakutenda mwujiza wowote kwao, isipokuwa kule kumwambia yule mwanamke siri yake katika maisha yake ya zamani. Walakini watu wengi walimpokea. Kwa ajili ya furaha yao walimwambia yule mwanamke: “Sasa tumeamini siyo kwa maneno yako, maana tumemsikia sisi wenyewe, na tunajua kuwa huyu ndiye Kristo hakika, Mwokozi wa ulimwengu.TVV 102.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents