Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Petro alichanganyikiwa

  Wanafunzi walifurahi kwamba Bwana wao aliyekuwa kama mtu aliyepotea, mpole, akitangatanga tu katika hali ya ufukara, sasa ametukuzwa na utukufu wa mbinguni. Waliamini kuwa Eliya amekuja kutangaza kusimamishwa kwa, ufalme hapa duniani. Kwa hiyo walitaka kukaa hapa. Petro alitamka, “Bwana, ni vizuri sisi kukaa hapa, na tujenge nyumba tatu; moja yako, moja ya Musa na moja ya Eliya.’ Wanafunzi waliamini kwamba Musa na Eliya wametumwa kuja kumlinda Bwana wao na kumsaidia kuimarisha ufalme wake.TVV 239.5

  Lakini ni kwamba, kabla ufalme haujasimamishwa, kwanza lazima uje msalaba. Yesu akivaa ubinadamu, akibeba mzigo wa huzuni zote na dhambi zote za wanadamu alitembeatembea kati ya wanadamu. Kadiri giza la mateso lililokuwa likimkabili, alikuwa na sikitiko kuu la rohoni, hasa akiwa katika ulimwengu usiomjua, hata wanafunzi wake wapendwa hawakuelewa kazi yake ulimwenguni. Katika ulimwengu aliouumba alikuwa mgeni kabisa asiyejulikana. Sasa mbingu ilikuwa imetuma wajumbe ambao si malaika, ila wanadamu waliovumilia na kupitia katika matatizo ya ulimwengu, yaani masikitiko ya kila aina, mateso, ambao ndio wanaomsikitikia Mwokozi.TVV 240.1

  Musa na Eliya wamekuwa wenzi wake Kristo. Wameshiriki kazi ya wokovu wa wanadamu. Musa aliwaombea Waisraeli akisema, “Walakini sasa ikiwa utawasamehe dhambi yao na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitaabu chako ulichoandika.’ Kutoka 32:32. Eliya alikuwa amejua sikitiko la moyo, jinsi alivyokuwa katika miaka mitatu na miezi sita ya njaa jinsi alivyochukuliana mashutumu na chuki ya taifa zima. Alikimbilia jangwani akiwa peke yake mwenye masikitiko makuu na kukata tamaa. Mzigo wao ulikuwa kuhusu wokovu wa binadamu.TVV 240.2

  Wanafunzi waliokuwa wamelala walisikia mambo machache tu ya maongezi ya wajumbe hao. Hawakusikia mambo Mungu aliyokusudia wasikie; yaani mateso ya Kristo na utukufu wa baadaye. Walipoteza mibaraka kabisa. Walakini walijua kwa hakika kuwa dhambi za Waisraeli za kumkataa Mwokozi zilikuwa dhahiri mbele za Mungu. Walipewa ujuzi kuhusu kazi ya Mkombozi. Walikuwa mashahidi wake, na kuona yote. 2 Petro 1:16. Walifahamu kwa dhahiri kuwa Yesu ndiye Masihi, kwamba ni Mfalme wa ulimwengu.TVV 240.3

  Walipokuwa wangali wakiangalia mambo hayo, wingu jeupe liliwafunikiza, tazama sauti ilitokea winguni ikisema: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye; msikieni yeye.’ Waliposikia sauti ya Mungu ikisema kwa ngurumo iliyotetemesha milima, wanafunzi waliangukia mbali katika nchi, hali wamefunika nyuso zao, mpaka Yesu alipowasogelea, na kutuliza hofu yao kwa kusikia sauti yake ambayo wameizoea. Akasema, “Simameni, msiogope.” Utukufu wa mbinguni umekwisha kupita. Sura za Musa na Eliya zimekwenda. Sasa walibaki peke yao na Yesu.TVV 240.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents