Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  68 — Wayunani Walipotaka “Kumwona Yesu”

  “Palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliokwenda kuabudu kwenye sikukuu. Basi hao walimwendea Filipo, wakamwomba wakisema Bwana, sisi tunataka kumwona Yesu. “Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.”TVV 349.1

  Kwa wakati huu kazi ya Kristo ilionekana kana kwamba itashindikana. Alikuwa ameshinda katika majadiliano na Mafarisayo na Makuhani, lakini ilikuwa dhahiri kuwa hangepokelewa, nao kama Masihi. Utengano wa mwisho ulikuwa umefikiwa. Ilionekana hakuna tumaini. Lakini jambo kubwa la kuhusu ulimwengu mzima lilikuwa karibu kutokea. Kristo aliposikia kwa hamu kwamba kuna watu “wanaotaka kumwona, Yesu” wakiwakilisha kilio cha ulimwengu, uso wake uling’aa kwa furaha, akasema: “Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu.”TVV 349.2

  Watu hawa walikuja kutoka Magharibi ili kumwona Mwokozi katika saa ya mwisho ya maisha yake. Mamajusi walikuja panapo mwanzo kutoka Mashariki. Wayunani hawa waliwakilisha mataifa, makabila na watu wa alimwengu mzima. Watu wa nchi zote na wa vizazi vyote watavutwa na msalaba wa Mwokozi.TVV 349.3

  Wayunani hao walitamani kujua ukweli kuhusu kazi ya Kristo. Wakati waliposema: “Tunataka kumwona Yesu,” Alikuwamo hekaluni, sehemu ile ambamo watu wengine wote isipokuwa Wayahudi hawakuruhusiwa, lakini Yesu aliwaendea Wayunani huko katika ukumbi wa nje akaongea nao binafsi.TVV 349.4

  Haja ya Wayunani ilimwonyesha Kristo kuwa dhabihu aliyekuwa anataka kutoa itawaleta wengi kuwa wana na binti za Mungu. Alifahamu kuwa muda si kitambo Wayunani watamwona wakiwa katika hali ambayo hawakudhania. Watamwona akiwekwa pamoja na Baraba, mnyang’anyi na muuaji. Kwa swali, “Basi, nimtendeeje Yesu?” Jibu litakuwa “Asulibishwe.”(Mathayo 27:22. Kristo alijua kuwa kwa kufanya, upatanisho ufalme wake utakamilika na kuenea katika ulimwenguni kote. Atakuwa Mtengenezaji, na Roho wake atashinda.TVV 349.5

  Kwa muda kitambo alisikia sauti zikitangaza katika sehemu zote za dunia “Tazama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu.” Yohana 1:29. Katika wageni hawa aliona ahadi ya mavuno makubwa. Tegemeo la haya, utimilivu wa tumaini lake ulionekana katika maneno haya; “Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu.” Lakini njia ya kufikia kutukuzwa huku haikuwa kujificha mawazoni mwa Kristo. Kwa kifo chake peke yake ndipo ulimwengu ungeokolewa. Kama punje ya ngano, Mwana wa Adamu hana budi kufukiwa ardhini afe na kuzikwa asionekane; lakini yapasa aishi tena.TVV 350.1

  “Amini, amin nawaambia chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa hutoa mazao mengi.” Chembe ya ngano inapoanguka chini na kufa, huchipua na kuzaa mazao. Hivyo ndivyo na kifo cha Kristo kitazaa matunda mengi katika ufalme wa Mungu. Kufuatana na kawaida ya asili ya mbegu za mboga uhai ulikuwa uwe matokeo ya kufa kwake.TVV 350.2

  Mwaka hadi mwaka mwanadamu huhifadhi pato la mbegu zake kwa kuzimwaga chini mbegu bora. Kwa muda lazima zifunikwe ardhini kuangaliwa na Bwana. Kisha huonekana jani, halafu mche, kisha mmea kamili ndipo chembe.TVV 350.3

  Mbegu iliyofunikwa udongoni huzaa tunda, halafu tunda nalo hupandwa, na hivyo mavuno huongezeka. Ndivyo hivyo na kifo cha Kristo msalabani, kitazaa matunda ya uzima wa milele. Kuitafakari kafara hii utakuwa utukufu kwa wale ambao kama tunda lake wataishi milele zote.TVV 350.4

  Kristo angeweza kujiokoa na kifo kama angechagua. Lakini kufanya hivyo angalibakia mwenyewe. Kwa kuanguka ndani ya udongo ili kufa ndiko kungeweza kuzaa matunda, yaani kuokoa watu wengi na kuwaingiza katika ufalme wa Mungu.TVV 350.5

  Fundisho hili la kujitoa kafara lazima lifunzwe kwa wote. “Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele.” Maisha lazima yazikwe katika mfereji wa haja za ulimwengu. Kujipenda nafsi, upendo wa nafsi lazima vipotee. Kanuni ya kujitoa ndiyo kanuni ya uzima. Kutoa ni kuishi. Maisha yatakayohifadhiwa ni yale yanayotumika katika kazi ya Mungu na kumhudumia mwanadamu.TVV 350.6

  Maisha yanayotumikia nafsi ni kama mbegu iliyoliwa. Hakuna ongezeko. Mtu anaweza kukusanya vitu vyote awezavyo; anaweza kuishi na kufikiri, na kujipangia awezavyo; lakini maisha yake hutoweka na wala hana kitu cho chote. Maisha ya ubinafsi ni maisha ya kujiangamiza.TVV 351.1

  Yesu anasema: “Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.” Wale wote waliochukua msalaba wa kujikana pamoja na Yesu, watakuwa washiriki utukufu pamoja Naye. Wao ni watenda kazi pamoja na Kristo, na Baba atawaheshimu jinsi anavyomheshimu , Mwanaye.TVV 351.2

  Ujumbe wa Wayunani ulileta mawazoni mwa Yesu kazi ya ukombozi tangu ilivyopangwa mbinguni, hadi kifo ambacho sasa kilikuwa kinakaribia sasa. Wingu la siri lilionekana kumfunika Mwana wa Mungu. Alishikwa na mawazo mengi. Baadaye ukimya ukaondolewa kwa sauti ya kilio. “Sasa roho yangu imefadhaika nami nisemeje Baba, uniokoe katika saa hii? Ubinadamu wake Kristo ulijikunyata kutoka katika saa ya kuachwa, wakati ambapo wote watamwona akipigwa na kuteswa. Alijikunyata kutoka katika hali ya kutendewa kama mhalifu mkuu wa wote, kutoka katika mauti ya fedheha. Mzigo mkubwa wa makosa ya walimwengu na ghadhabu ya Baba kwa sababu ya dhambi za ulimwengu vilisababisha roho ya Yesu kuzimia, na hofu ya mauti kuutanda uso wake.TVV 351.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents