Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siri ya mambo yake ya nyuma

    Sasa Yesu aligeuza maongezi yake ghafla. Mwanamke huyu apaswa kupokea karama ambayo Yesu anatamani kuitoa, yaani lazima afahamu makosa yake na amfahamu Mwokozi wake pia. Yesu alimwambia, “Nenda ukamwite mume wako, mje naye hapa.” Mwanamke akajibu, “Sina mume.” Lakini Mwokozi akaendelea kusema, “Umesema vema kwamba sina mume, maana una waume watano, na yule uliye naye siye mume wako. Umesema kweli.”TVV 98.7

    Mwanamke alitetemeka. Mkono wa siri ulikuwa unafunua kurasa za maisha yake. Ni nani huyu anayeweza kugundua siri ya maisha yake? Mawazo yakamjia ya mambo ya milele, na hukumu ya mwisho, wakati siri zote zitakapofichuliwa. Alijaribu kupiga chenga, lakini alishindwa. Basi akasema: “Bwana naona kwamba wewe u nabii.” Halafu akitaka kukomesha mazungumzo, aligeukia mambo ya dini.TVV 99.1

    Kwa uvumilivu Yesu alingojea nafasi ya kumweleza ukweli kamili. Mwanamke alisema, “Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi mwasema kuwa, Yerusalemu ndipo mahali pa kuabudu.” mlima wa Gerizimu ulikuwa unaonekana, ambao ndio uliokuwa ukishindaniwa baina ya Wayahudi na Wasamaria. Kwa muda wa miaka mingi Wasamaria walijichanganya na waabudu sanamu, kwa hiyo dini yao ikapotoshwa na kuharibika kabisa; watu wote wakaharibika.TVV 99.2

    Wakati hekalu la Yerusalemu lilipojengwa na Ezra, Wasamaria walitaka kuungana na Wayahudi ili wajenge mji. Jambo hili lilikataliwa, kwa hiyo uadui ukaibuka kati ya mataifa hayo mawili. Wasamaria walijenga hekalu juu ya mlima wa Gerizimu kwa kushindana na Wayahudi. Lakini hekalu lao liliharibiwa na maadui, wakaonekana kama wamelaaniwa. Walakini hawakuliamini au kulikubali hekalu lililokuwa Yerusalemu; kama ni nyumba ya Mungu, wala hawakukubali kuwa dini ya Wayahudi ilikuwa dini bora.TVV 99.3

    Yesu akimjibu mwanamke, alisema: “Saa inakuja ambayo hamtaabudu katika mlima huu, wala Yerusalemu. Mnaabudu msichojua, sisi tunaabudu maana wokovu unatoka kwa Wayahudi.” Sasa Yesu alitaka kuondoa uhasama huu baina ya Wasamaria na Wayahudi. Ukweli mkuu wa wokovu ulikuwa umekabidhiwa kwa Wayahudi, na kutokana na wao Masihi atatokea.TVV 99.4

    Yesu alitaka kuinua mawazo ya mwanamke huyu yaondoke katika mambo ya ushindani. Akasema: “Saa inakuja, na sasa ipo, ambayo wamwabuduo Baba halisi watamwabudu katika roho na kweli, maana Baba atafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, na watu wamwabuduo yeye inawapasa kumwabudu katika roho na kweli.”TVV 99.5

    Watu hawaletwi mbnguni kwa njia ya mlima mtakatifu, au kwa hekalu takatifu. Ili tupate kumwabudu Mungu sawasawa, hatuna budi kuzaliwa kiroho kutoka juu. Jambo hili litatakasa moyo na kuimarisha dhamiri, na kutuwezesha sisi tutembee katika utii wa maagizo yake. Hii ndiyo ibada ya kweli. Haya ndiyo matunda ya utendaji wa Roho ndani yetu. Mtu yeyote anapomtafuta Mungu kikweli, utendaji wa Roho Mtakatifu huonekana, na Mungu hujidhihirisha kwa mtu huyo.TVV 100.1

    Mwanamke alipokuwa akizungumza naye, maneno ya Yesu yalimwingia. Maisha yake ya zamani yalipofunuliwa wazi, akaona kiu ya haki moyoni mwake, ambavyo maji ya kisima cha watu hayawezi kumaliza. Hakuna kilichovuta usikivu wake kuliko hiki. Ingawa Yesu alimtobolea siri zake, walakini alimhesabu kuwa rafiki yake, anayemhurumia na kumpenda. Ijapokuwa utakatifu wa Yesu umefunua dhambi zake, lakini Yesu hakutamka neno lolote la kumlaumu kwa ajili ya dhambi hiyo, Yesu amekuwa akiongea juu ya neema iwezayo kutakasa moyo wake. Swali alilouliza kuhusu Masihi lilisahauliwa, vile alihisi kuwa ni yeye. Alisema: “Najua kuwa Masihi, ambaye ni Kristo, akija atatueleza yote.” Yesu akasema “Mimi nizungumzaye na wewe ndimi Masihi.”TVV 100.2

    Mwanamke aliposika maneno hayo imani ilichemka rohoni mwake. Akakubaliana na usemi wote uliosemwa na Mwalimu wa mbinguni.TVV 100.3

    Moyoni mwa mwanamke huyu kulikuwa na furaha sana. Alipendezwa na maandiko matakatifu. Roho Mtakatifu alikuwa akimtayarisha kupokea ukweli mwingi zaidi. Unabii wa Agano la Kale ulikuwa ukimulika moyoni mwake. Maji ya uzima ambayo Kristo humpa kila mwenye kiu, yalikuwa yakianza kububujika moyoni mwake.TVV 100.4

    Maelezo ya wazi yaliyoelezwa na Kristo kwa mwanamke huyu, yasingalielezwa na Wayahudi wanaojiona kuwa haki machoni pao. Mambo hayo yamefichika kwao, na wanafunzi wanayachuchumilia. Hayo yamefunuliwa kwa mwanamke huyu. Yesu akamwona kuwa atashirikiana na wengine furaha hii pia.TVV 100.5

    Wanafunzi wake waliporudi, walishangaa kumwona Mwalimu wao anazungumza na mwanamke. Hakungoja kula chakula kilicholetwa na wanafunzi. Mwanamke alipokwisha kwenda, wanafunzi walimsihi Yesu ale chakula. Walimwona akiwa kimya na uso wake ukingaa. Waliogopa kumwingilia, huku wakifikiri kuwa si vema kunyamaza bila kumpa chakula. Yesu akielewa watakavyo, alisema, “Nina chakula ambacho ninyi hamkijui.TVV 100.6

    Wanafunzi wakawa na wasiwasi, kuwa ni nani aliyemletea chakula! Halafu Yeye alisema: “Chakula changu ndicho hiki, kuyafanya mapenzi yake yeye aliyenipeleka, na kuimaliza kazi yake.” Kumhudumia mtu aliyekuwa na njaa na kiu ya ukweli wa Mungu, ulikuwa muhimu yake kuliko kula chakula; au kunywa maji.TVV 101.1

    Mwokozi wetu alitamani kuwashughulikia na kuwafadhili watu ambao aliwanunua kwa damu yake. Kama vile mama anavyofurahia kicheko cha mtoto wake anayekua, ndivyo Kristo anavyofurahia yule anayekua kiroho.TVV 101.2

    Mwanamake yule alijazwa na furaha alipokuwa akiyasikiliza maneno ya Kristo. Aliuacha mtungiwake pale, akarudi mjini ili kupasha habari hizi kwa wengine. Alisahau mambo ya kuchota maji, na kiu ya Kristo aliyotaka kushughulikia. Kwa furaha iliyojaa moyoni mwake aliharakisha kwenda kuwapasha wengine juu ya nuru aliyopokea.TVV 101.3

    Alipaaza sauti akisema: “Njooni mwone mtu aliyeniambia mambo yangu niliyofanya.” “Je huyu siye Kristo?’ Alikuwa na mabadiliko usoni pake, na hali yake ilichangamka sana. Wakatoka mjini wakamwendea.TVV 101.4

    Yesu alipokuwa angali akiketi pale kisimani, aliangalia uwanda ulioenea mbele yake umejaa nafaka pevu iliyokomaa. Akinyosha mikono yake kuuelekea, alisema kwa mfano: “Hamsemi ninyi, Imebaki miezi minne ndipo yaje mavuno? Angalieni nawaambia, Inueni macho yenu, mkayatazame mashamba, kwa maana yamekuwa meupe tayari kwa mavuno. Hapa yalikuwako mavuno tayari kwa kuvunwa.TVV 101.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents