Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Shetani alivyokuwa karibu kufaulu

  Utimilifu wa wakati umekuja. Ubinafsi umedhiliwa kwa muda mrefu, kwa ajili ya maasi, ya kukutazamia kuja kwa Mkombozi. Shetani alikuwa akijitahidi kufanya shimo la kuvukia liwe refu zaidi, ili isiwezekane kuvuka kutoka duniani hata mbinguni. Amewaingiza watu dhambini. Ilikuwa nia yake kufanya uvumilivu wa Mungu ukome, hata awaachilie watu mbali katika mikono ya Shetani.TVV 19.2

  Juhudi ya Shetani ya kuutwaa ulimwengu karibu ilifaulu. Ni kweli kwamba katika kila kizazi, hata katika mataifa, kulikuwa na watu wenye kumcha Mungu. Lakini watu hawa walichukiwa sana. Wengi wao wlaiteseka sana kiasi cha kuuawa. Giza hilo ambalo Shetani alilitia ulimwenguni lilizidi kuwa kubwa zaidi.TVV 19.3

  Shetani alishinda vita katika kuwapotosha Waisraeli, wasiwe na imani. Wakafiri walikosa wa kuwafundisha, kwa hiyo wakazidi kuharibika. Kosa ni la Waisraeli. Kanuni ya kutegemea matendo mema ili yampatie mtu nafuu, ni kanuni ya dini za kikafiri. Kanuni hiyo iliingia hata kwa Waisraeli, ikawa ndiyo dini yao.TVV 19.4

  Wayahudi wameudanganya ulimwengu kwa kuwapa dini ya kuiga, ambayo ni potofu. Wamekataa kujitoa kwa Mungu kamili, ili wawape walimwengu wkovu, badala yake wamekuwa vyombo vya Shetani kuwaharibu. Watu ambao waliitwa na Mungu wawe nguzo na msingi imara, wamegeuka kuwa watenda kazi wa Shetani, wakiukosesha ulimwengu, uone kwamba mungu hana haki, ila ni mdanganyifu. Makuhani hekaluni walipotosha kazi ya ukuhani. Utaratibu uliowekwa na Mungu mwenyewe, ukageuzwa kuharibu watu na kuwapofusha tu. Mungu hana la kumfanyia mtu zaidi kwa njia hii.TVV 19.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents