Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    44 — Ishara ya Kweli

    Huko Dekapoli mahali ambao mwenye pepo aliponywa, na wenyeji wakamlazimisha Yesu aondoke kwao. Lakini walikuwa wamewasikiliza wajumbe aliowaacha huko. Yesu alipokwenda katika sehemu hiyo tena, kundi kubwa lilikusanyika kwake, na mtu bubu na kiziwi aliletwa kwake. Yesu akimtenga kando, aliweka vidole vyake katika masikio yake, na kuugusa ulimi wake. Alipiga kite kana kwamba masikio hayo hayatafunguka ili kuisikia kweli, na ulimi umeikataa kweli; na kumkataa Mwokozi. Aliposema, “Funguka”, mtu akapona.TVV 226.1

    Yesu akapanda mlimani, na huko makutano walimkusanyikia, wakiwaleta wagonjwa wao na vilema, akawaponya wote. Watu walimtukuza Mungu ingawa walikuwa wamizimu. kwa muda wa siku tatu walikuwa na Mwokozi, huku wakilala nje mbugani tu, wakiwa na hamu ya kuyasikiliza maneno ya Mwokozi, na kuziona kazi zake.TVV 226.2

    Baada ya siku tatu kupita chakula walichokuwa nacho, kiliwaishia. yesu asingaliwaaga waende zao, na njaa, kwahiyo akawaambia wanafunzi wake wawapatie chakula. Huko Bethsaida waliona jinsi chakula kidogo kilivyotosha kuwalisha makutano mengi, walakini sasa hawakuweza kukumbuka mambo hayo na kutoa chochote walichokuwa nacho, ili kwa uwezo wake kitoshe kuwalisha watu. Lakini hata wakati huu wanafunzi walionyesha imani haba. Watu waliolishwa huko Bethsaida walikuwa Wayahudi, lakini hawa ni watu wa mataifa. Hali ya ubaguzi ilikuwa bado kali kwa wanafunzi. Kwa hiyo walisema: “Tutapata wapi chakula cha kutosha watu wote hawa nyikani hapa?”TVV 226.3

    Lakini kwa kutii neno lake, walileta walichokuwa nacho, ambacho ni mikate saba na samaki wawili. Basi hivi viliwalisha makutano, na kubakiza makapu saba. Jumla ya watu walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto.TVV 226.4

    Kisha Yesu na wanafunzi wake walivuka ziwa mpaka Magdala. Sehemu hii ya Tiro na Sidoni roho yake iliburudika kwa habari ya mwanamke wa Kifoeniki. Watu wa mataifa wa Nikapoli wamempokea kristo kwa furaha. Sasa walipofika tena Galilaya, ambako kazi zake nyingi zilifanyika, alipokewa kwa unyonge sasa.TVV 227.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents