Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    49 — “Mtu Akiwa na Kiu, na Aje”

    Wayahudi walipaswa kukutanika huko Yerusalemu mara tatu kwa mwaka kwa makusudi ya dini. Kusanyiko la Siku kuu ya Vibanda lilikuwa la mwisho kwa mwaka. Mavuno yalikusanywa katika mbuga na mabonde. Matunda ya kutoa divai yalikuwa yanachumwa.TVV 253.1

    Sikukuu iliendelea muda wa siku saba. Watu wengi wa Palestina na kutoka sehemu nyingine walikusanyika huko Yerusalemu. Wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa masikini, wote walikuja wakiwa na vipaji vyao vya shukrani kwa Mungu aliyewabarikia katika mwaka, kwa ajili ya wema wake. Kila jambo lililoleta furaha lilitendeka, ili kuonyesha wema wake. Mji ulipambwa kwa mapambo yote.TVV 253.2

    Sikukuu haikuwa kwa ajili ya shukrani ya mavuno peke yake, ila ya ukumbusho wa ulinzi wa Mungu kwa wana wa Israeli jangwani. Katika maadhimisho ya maisha yao ya kuishi mahemani katika sikukuu ya vibanda vilivyojengwa kando ya hekalu. Vilima na mabonde vilivyojengwa vinazunguka Yerusalemu ilienezwa na vibanda hivi vya majani. Wenye kuabudu waliimba nyimbo takatifu walipokuwa wakisherehekea sikukuu hii.TVV 253.3

    Kitambo kabla ya sikukuu hii ilikuwa Siku ya Upatanisho, ambaya iliwalazimu watu kurekebisha maisha yao kama mbingu inavyotaka. “Mshukuruni Bwana... kwa kuwa rehema zake zakaa milele.”(Zaburi 106:1). Ilikuwa shangwe kuu, na watu wote walishirikiana katika kuimba na kusifu.TVV 253.4

    Hekalu ndiyo ilikuwa kiini cha furaha. Pande zote za ngazi za hekaluni ambazo ni zenye mawe yang’aayo waimbaji wana wa Lawi ndio walioongoza huduma, ya nyimbo. Sauti ilisikika kwa mbali sana, hata sifa za kusifu zikaenea mahali popote.TVV 253.5

    Wakati wa usiku hekalu liliangazwa kwa mwanga wa mishumaa na vimuli vilivyotengenezwa, nyimbo, kuyumba kwa matawi ya mitende na umati wa watu uliowasha taa na mienge, pamoja na maadhimisho ya sikukuu, ilifanya hali ya mambo iwe ya kupendeza mno. Lakini jambo la kuvutia zaidi lilikuwa ni ule ukumbusho wa safari ya jangwani.TVV 253.6

    Wakati kunapambazuka, makuhani walipiga tarumbeta zao, na watu wote vibandani waliitikia kwa shangwe kuu. Kisha makuhani wakachovya maji ya kijito cha Kedron yaliyokuwa yakitiririka na kuyanyunyiza kwenye ngazi za hekalu, wakifuatisha mlio wa wimbo, na kufanya jambo lionekane kuwa la kupendeza mno.TVV 254.1

    Katika kibweta cha Makuhani kulikuwako na mabeseni mawili ya fedha. Mojawapo lilijazwa maji, na gudulia la mvinyo kwa jingine. Na yote mawili mawili yalifunika kabisa na kutiririka mpaka mtoni na baharini. Maji haya matakatifu yalifananishwa na ile chemchemi ya maji iliyofurika kutoka mwambani na kuwanywesha Waisraeli jangwani, ambayo iliamuriwa na Mungu.TVV 254.2

    Wana wa Yusufu walipojiandaa kuhudhuria katika sikukuu waliona kuwa Kristo hakuondoka, au kutoka toka wakati wa kuhudhuria. Tangu alipomponya mgonjwa huko Bethsaida, hakuhudhuria tena katika sikukuu za kitaifa. Aliendelea kufanya kazi yake huko Galilaya ili kuepukana na mashindano na Wayahudi huko Yerusalemu. Kule kuonekana kwake kana kwamba hajali mikusanyiko ya dini kama wengine, kuliwafanya makuhani na marabi wamchukie na kumfanyia uhasama, jambo hili lilileta wasiwasi hata kwa jamaa yake pia. Katika mafundisho yake alisisitiza juu ya utii, lakini yeye mwenyewe alionekana kana kwamba hajali mambo yaliyoamuriwa na Mungu, kuhusu huduma za mikusanyiko.TVV 254.3

    Hali yake ya kushirikiana na watoza ushuru na kutofuata maagizo ya marabi; na kutojali mapokeo ya wazee kuhusu kutunza Sabato, yote hayo yalimfanyia uhasama mkubwa kwa waongozi wa dini. Ndugu zake walisema kuwa ni kosa sana kuwapinga wakuu jinsi hii, hali ni watu waliojifunza sana, na kuheshimiwa na wote. Waliona kuwa watu hawa walikuwa sawa, Yesu ndiye mwenye makosa. Lakini walikuwa na matataniko, walipomwona Yesu jinsi anavyoishi bila makosa kama watu wengine, na kazi yake ya ajabu. Walitumaini kuwa atawaaminisha Wayahudi kuwa yeye ndiye Masihi, Mkuu wa Israeli. Walijivunia wazo hili.TVV 254.4

    Hiyo ndiyo ilikuwa haja yao, kwa hiyo walimkazania Yesu aende Yerusalemu. Walisema: “Ondoka hapa”. Uende Uyahudi, ili wanafunzi wako nao wapate kuziona kazi zako. Maana hakuna mtu atendaye jambo kwa siri, na yeye pia alitaka kujulikana. Ukifanya mambo haya, yafanye waziwazi ulimwenguni. Akijua kuwa ni yeye Masihi kwa nini kujificha? Kwa nini haendi huko Yerusalemu kijasiri na kutenda matendo haya yanayosemwa huko Galilaya? Walis-ema, “Usijifiche huku katika jimbo la Galilaya, mahali pasipojulikana wazi. Jidhihirishe huko katika makao makuu, ukaungwe mkono na Makuhani na wakuu, ili upate kuusimamisha utawala wako.TVV 254.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents