Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    77 — Kristo Ashtakiwa Mbele Ya Gavana Wa Kirumi

    Katika jumba la hukumu, la Pilato, Gavana wa Kirumi, Kristo alisimama akiwa amefungwa kama mahabusi, huku akilindwa na askari. Jumba lilikuwa limeanza kujaa watazamaji. Nje walisimama mahakimu wa baraza kuu la Kiyahudi (Sanhedrini), makuhani, wakuu na watu wenye ghasia.TVV 408.1

    Baada ya kumhukumu Yesu kifo wajumbe wa Sanhedrini, walifika kwa Pilato, ili aithibitishe hukumu na kuitekeleza. Lakini maofisa wa Wayahudi hawakupenda kuingia katika jumba la hukumu la Kirumi. Kwa kufuata kanuni zao, wangekuwa najisi na hivyo washindwe kushiriki katika Pasaka. Wao hawakuona kuwa kule kuwa na chuki ya kuua juu ya Yesu kulitia najisi katika mioyo yao. Wala hawakuona kuwa kwa vile walikuwa wamemkataa Kristto Mwana kondoo halisi wa Pasaka, siku kuu ile ilikuwa imepoteza maana yake kwao.TVV 408.2

    Pilato alimtazama Mwokozi kwa jicho baya. Akiwa ameitwa kwa haraka kutoka usingizini alikusudia kufanya kazi yake kwa haraka ilivyowezekana. Akikaza macho, kwa hasira yake yote, aligeuka kuona ni mtu wa namna gani aliyeletewa kuhoji. Alimkazia Yesu macho kwa makini. Alikuwa akishughulika na aina zote za wahalifu, lakini kamwe alikuwa hajaletewa mtu mwema, mwungwana, mtulivu, kama huyu. Usoni mwake hakuona dalili yo yote ya uhalifu, wala hofu, ushupavu au kutaka shari. Alimwona mtu ambaye uso wake ulikuwa na sura ya mbinguni.TVV 408.3

    Mtazamo wa Kristo ulimfanya mguso wa pekee kwa Pilato asili yake iliamushwa. Alisha wahi kusikia habari za na matendo ya Yesu. Mke wake alikuwa amemsimulia matendo bora ya nabii huyu wa Galilaya, aliyekuwa akiponya wagonjwa na kufufua wafu. Alikumbuka tetesi alizosikia kutoka kwa watu mbali mbali. Aliwataka Wayahudi waeleze madai yao dhidi ya mshtakiwa. Mtu huyu ni nani, na kwa nini ameletwa? Walijibu kwamba alikuwa mlaghai aliyeitwa Yesu Mnazareti.TVV 408.4

    Tena Pilato akawauliza: “Ni mashitaka gani mnayoleta juu ya mtu huyu?” Makuhani hawakujibu swali lake, ila walisema kwa hasira “Kama huyu asingekuwa mtenda mabaya tusingemleta kwako.” Wakati baraza kuu la Kiyahudi (Sanhedrini) linapomleta mtu kwako huwa astahiliye kuuawa, kuna haja gani kuuliza kuwa mnamshitakia nini? Walitumaini kumfanya Pilato aridhike tu bila kufanya uchunguzi zaidi.TVV 409.1

    Kabla ya haya, Pilato alipata kuidhinisha kwa haraka hukumu ya kifo kwa watu wasiyostahili kifo. Kwake yeye kama mshitakiwa ana hatia au hana hatia halikuwa jambo kubwa. Makuhani walitumaini kuwa sasa Pilatto ataidhinisha adhabu ya kifo dhidi ya Yesu bila ya kumsikiliza.TVV 409.2

    Lakini kitu fulani ndani ya mshitakiwa kilimfanya Pilato asite. Hakuthubutu kufanya hivyo. Alikumbuka jinsi Yesu alivyomfufua Lazaro, mtu aliyekuwa amezikwa kaburini siku nne; na hivyo alitaka kujua mashtaka dhidi yake na kama yaliweza kuthibitishwa.TVV 409.3

    Alisema kama hukumu yenu ni kamili, kwa nini mmemleta kwangu? “Haya mtwaeni ninye makamhu-kumu kwa ile torati yenu!” makuhani walisema kuwa wao wamemaliza kumhukumu tayari, lakini ni lazima wapate idhini ya Pilato ili kufanya hukumu iwe halali. Pilato akauliza: “Mlimhukumu nini? Wakajibu “Kufa.” Walitaka Pilato aidhinishe adhabu waliyotoa, na lo lote litakalotokea ni juu yao. Licha ya udhaifu wake kiroho Pilato alikataa kumhukumu Yesu mpaka asikie mashtaka juu yake.TVV 409.4

    Makuhani walijikuta katika utata. Hawakutaka ijulikane kwamba Kristto amekamatwa kwa sababu za dini, maana hayo hayatakuwa na uzito wowote kwa Pilato. Lazima waonyeshe madai kuwa mashtaka yake yanahusu mambo ya siasa. Warumi waliangalia sana mapinduzi yasitokee. Katika hatua za mahangaiko yao ya mwisho, makuhani wakawaita mashahidi wa uongo. Waliosema: “Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme.” Mashitaka matatu, kila moja lisilo na msingi wo wote. Makuhani walijua hivyo lakini walikuwa tayari kushuhudia uongo.TVV 409.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents