Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  9 — Matatizo ya Kristo Wakati wa Utoto

  Katika shule za masinagogi, wanafunzi wakiwa chini ya waalimu wa Kiyahudi, walifundishwa kushika kawaida zisizokuwa na hesabu kwa wingi, ambazo kuhesabiwa kuwa ndizo za dini kamili, zenye kuonyesha kuwa watu hawa ni washika dini hasa. Lakini Yesu hakushughulika na mambo kama hayo. Tangu utoto wake, Yesu hakuhangaika na kawaida hizo. Maandiko matakatifu ndiyo yalikuwa masomo yake ya kawaida, na maneno, “Ndiyo asemavyo Bwana”, ndiyo yalikuwa kinywani mwake daima.TVV 41.1

  Aliona kuwa watu walikuwa wakijitenga na neno la Mungu, ila tu wakishika kawaida ambazo hazina faida yoyote. Katika huduma zao ambazo si za imani, hazikuwaletea utulivu rohoni mwao. Hawakujua uhuru wa roho unaoletwa na neno la Mungu linapoaminiwa. Ingawa Yesu hakukubaliana na halli hiyo kuchanganya neno la Mungu, na hadithi za kibinadamu, walakini hakuwashambulia walimu hao, wala kawaida zao. Walipomlaumu kwa hali yake tofauti na wao, alileta neno la Mungu kuwa ndiyo msimamo wake.TVV 41.2

  Yesu alijaribu kuwapendeza wale aliokutana nao. Kwa kuwa alikuwa mtu mwungwana sana, waandishi na wazee walidhani kuwa ataweza kugeuzwa upesi na kufuata kawaida zao. Lakini aliwauliza mahali wanaposoma katika maandiko, mambo hayo. Yeye alitii kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu, lakini hadithi za wanadamu hakuzijali. Yesu alionekana kujua Maandiko kutoka mwanzo mpaka mwisho, naye aliyatumia katika ukweli wake. Walimu wa Kiyahudi, yaani walimu wakuu, walijidai kuwa wao ndio wawezao kuyafafanua Maandiko katika ukweli wake. Walijua kuwa wasingeweza kupata neno katika mandiko liwezalo kukubaliana na mambo yao. Hata hivyo walichukizwa kwa sababu Yesu alipingana nao. Walipokosa kumvuta Yesu, waliwaambia wazazi wake kuhusu ukaidi wa mtoto wao, hivyo Yesu akakabiliwa na magombezo ya Yusufu na Mariamu.TVV 41.3

  Tangu utoto wake, Yesu alianza kujitegemea na kujenga tabia yake. Kulitii Neno la Mungu, kulikuwa jambo muhimu kwake, kuliko neno lolote, hata upendo kwa wazazi wake haukuweza kumgeuza, asitii Neno la Mungu. Lakini hali ya walimu wakuu kulimsikitisha sana, akawa na huzuni katika maisha yake, Alijifunza fundisho gumu la kukaa kimya na kuvumilia sana.TVV 42.1

  Ndugu zake, yaani wana wa Yusufu waliungana na walimu wa Kiyahudi. Waliyaheshimu mapokeo ya wanadamu zaidi kuliko neno la Mungu, na walimlaumu Yesu kuwa ni mkaidi. Lakini ujuzi wake uliwashangaza marabi kwa jinsi alivyokuwa na majibu yake. Walakini hawakujifunza kuwa alikuwa akiwafundisha. Walitambua kuwa aliwazidi katika ujuzi, wala hawakuelewa kuwa asili ya ujuzi wake ni wapi.TVV 42.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents