Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Siri ya Uwezo wa Binafsi

  Yesu aliongeza kusema; “Msifurahi kwa kuwa pepo wanawatii kwa jina langu, ila furahini kwa kuwa majina yenu yameandikwa mbinguni.” Angalieni ubinafsi usiwaingilie mkafanya kazi kwa nguvu zitokanazo na ninyi wenyewe. Ubinafsi uko tayari kuwaingilia, mkadhani kuwa kufaulu kazi ni kutokana na nguvu zenu wenyewe. Tunapotambua udhaifu wetu, hatuna budi kutegemea nguvu ambazo sio zetu. Tazama 2 Wakorintho 12:10. Hakuna kitu kinachotusukuma katika utendaji wetu kwa hakika kama upendo wa Kristo. Lazima tushirikiane na Mungu, ndipo atatuvuvia Roho wake atakayetuwezesha kuwafikia wanadamu wenzetu. Kadiri utakavyoambatana na asili ya uwezo wote na nuru, ndipo utakuwa na uwezo zaidi wa kufanya kazi ya Mungu.TVV 278.4

  Jinsi wale sabini walivyomsikiliza Kristo, Roho Mtakatifu alivyoandika ukweli mioyoni mwao. Na kadiri makutano ya watu walivyokuwa wakiwazunguka, walikuwa kama wamefungwa ndani ya Mungu.TVV 279.1

  Yesu akijua ya kuwa wamevuviwa na uwezo wa juu, alisema: “Nakushukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima, ukawafunulia watoto wachanga, maana ndivyo ilivyokupendeza wewe.”TVV 279.2

  Wenye heshima na wakuu wa dunia hii, hawakuweza kutambua tabia ya Kristo. Ila wavuvi na watoza ushuru ndio waliofunuliwa mambo yasiyoonekana. Kila mara walipojitolea kwa Roho Mtakatifu na uwezo wake, mioyo ya wanafunzi iling’arishwa na uwezo wa mbingu. Wakatambua kuwa Mwenyezi Mungu aliyejivika katika ubinadamu, yuko pamoja nao. Kila mara alipoeleza mambo ya Agano la Kale na kutaja mambo yanayomhusu Yeye, walikuwa wakijisikia kuwa katika hali ya mbinguni. Walikuwa na ufahamu wazi kuliko walioyaandika. Hivyo waliweza kusoma maandiko ya Agano la Kale kama ni mafunuo mapya kutoka kwa Mungu. Walimwona yule ambaye ulimwengu haumjui.” Yohana 14:17.TVV 279.3

  Njia moja tu ambayo tutaweza kufaulu kupata ujuzi kamili wa ukweli ni kunyenyekeza mioyo yetu na kujiweka chini ya Roho ya Kristo. Elimu ya sayansi ya wanadamu ni ndogo nno kuweza kufahamu mpango wa ukombozi. Filosofia haiwezi kuueleza mpango wa ukombozi. Lakini sayansi ya ukombozi yaweza kujulikana kwa maisha yenvewe. Mtu anayeona maisha yake ya dhambi ndiye atafahamu thamani ya Mwokozi.TVV 279.4

  Yesu alikuwa akifundisha mafundisho kamili alipokuwa akienda Yerusalemu. Katika sehemu ya Perea watu hawakushikwa sana na mambo ya makuhani, kwa hiyo mafundisho ya Yesu yaliwaingia zaidi mioyoni.TVV 279.5

  Katika miezi ya mwisho, ndipo mifano mingi ya Yesu ilinenwa. Makuhani na Marabi hawakuweza kuipotosha. Walakini haikuwafaidia ipasavyo, ila waliendelea na mpango wa uhasama. Kristo aliutoa mfano safi wa kondoo aliyepotea na akautafsiri wazi na kusoma juu ya fedha na mwana mpotevu. Baada ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu wanafunzi, walipokwenda kazini, wakikabiliana na mashutumu na umaskini, na mateso, kila mara walijipa moyo walipokuwa wakikumbuka mafundisho hayo ya safari ya mwisho. “Msiogope enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapeni ufalme. Viuzeni mlivyo navyo, mtoe sadaka. Jifanyieni mifuko isiyochakaa akiba isiyopungua katika mbingu mahali pasipokaribia mwizi, wala nondo haharibu. Kwa kuwa hazina yenu ilipo ndipo itakapokuwa na mioyo yenu.” Luka 12:32-34.TVV 279.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents