Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uwezo wa kupambanua Wema na Ubaya

  Mungu hawalazimishi watu kuamini. Amekusudia kuwa watu wasiamini kijuujuu tu, ila waamini kwa hakika hasa wakiwa na uthibitisho wa maandiko matakatifu. Kama Wayahudi wangalipima na kulinganisha unabii na matukio, wangalifahamu kamili wakati wao na kuja kwa mtu wa Galilaya aliye mpole na mnyenyekevu.TVV 260.1

  Watu wengi leo hujidanganya kama Wayahudi walivyojidanganya. Walimu wa dini husoma Biblia na kuitafsiri kufuata mawazo yao, sawa na mapokeo yao, wala hawasomi Biblia na kujipima walivyo ila hujitolea kufuata tu walimu wanavyowaongoza. Mtu yeyote anayejifunza Biblia kwa nia hasa na maombi, ili apate kuongozwa nayo, atapata ufahamu wa mbinguni. Ataifahamu Biblia, “Mtu yeyote apendaye kufanya mapenzi yake, atafahamu kama mafundisho haya yatoka kwa Mungu au ninanena mambo yangu mwenyewe.”TVV 260.2

  Siku ya mwisho ya sikukuu, watu waliotumwa ili kumkamata Yesu, walirudi bila kuwa naye. Wakuu wao waliwauliza kwa hasira wakisema, “Mbona hamkumkamata?” Wao walijibu wakisema, “Kamwe mtu hajanena kama anenavyo mtu huyu.”TVV 260.3

  Walipozwa mioyo yao migumu kwa maneno haya. Walakini Yesu alipokuwa akinena walimsogelea wapate kushika kitu katika maneno yake cha kumshitaki lakini walipomsikiliza, walimwamini. Waliona kile ambacho makuhani na wazee hawakukiona. Mioyo yao ilijaa na maarifa ya Mungu.TVV 260.4

  Makuhani na wakuu walipofika mbele ya Yesu walijisikia vile vile. Roho zao ziliwaka, nao wakakubali kuwa, “Kamwe mtu hajanena kama anenavyo mtu huyu.” Lakini mara wakazidi kuwa wagumu wa mioyo, mpaka wakasema, “Je, hata ninyi mmedanganyika? Ni nani katika makuhani au wazee waliomwamini? Lakini watu hawa wasiojua sheria wamelaaniwa, ndiyo sababu wanamwamini.” Kwa wale ambao ukweli huhubiriwa kwao, mara chache huuliza, “Je, ni kweli? bali husema, “Unahubiriwa na nani?”TVV 260.5

  Watu wengi huupima ukweli huu kwa kuona watu walioamini, lakini swali linabaki kuwa, “Je, kuna wasomi au wakuu walioamini?” Haidhuru kuwa ni wangapi walioamini, au wasomi wangapi Wanaamini au wakuu wa dini walioamini. Swala lilidumu kuwa, kama Yesu akiachwa vivi hivi, aendelee tu, atawapotosha watu waache dini iliyokwisha kusimama. Njia moja ya kufanya ni kumkomesha asiendelee na mambo haya, mara moja. Katika mazungumzo yao ya mipango walivurugika kwa njia ya swali lililoulizwa na Nikodemo kwamba: “Je, sheria yetu inaruhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kumwona afanyavyo?” Wote walinyamaza kimya, maana hairuhusiwi kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza kwanza. Lakini walishupaza na kuona kwamba kuna mtu mmoja kati yao anayemtetea. Wakasema, “Je, na wewe ni mtu wa Galilaya pia?TVV 261.1

  Tafuta utaona kuwa hakuna nabii atokaye Galilaya. Walakini kwa ajili ya upinzani huo, wakuu walitulia kidogo, “Kila mtu akaenda nyumbani kwake.”TVV 261.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents