Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Jinsi Roho Mtakatifu alivyojaribu kuwasaidia

  Katika mkutano huu wa kupanga jinsi ya kumwua Kristo, shahidi aliyesikia majivuno ya mfalme Nebukadneza, na kusikia sikukuu ya sanamu ya Belshaza aliwasisitizia waone kazi zao na matokeo yake. Mambo katika maisha ya Kristo yamewatokea na kuwaonya kuhusu hali zao. Wanakumbuka wakati alipokuwa mtoto wa miaka kumi na miwili alisimama mbele ya walimu wakuu wa sheria, akiwauliza maswali yaliyowatatanisha. Mwujiza uliofanyika wa kumfufua Lazaro, unaonyesha kuwa Yesu si mtu wa kawaida, ila ni Mwana wa Mungu. Wazee wa baraza waliulizana kwa wasiwasi, wakisema: “Tufanyeje sasa?’ Baraza liligawanyika.TVV 303.3

  Baraza lilipokuwa na wasiwasi mkubwa, Kayafa, ambaye ndiye kuhani mkuu alisimama, mwenye kiburi, na mkatili, alisema kwa ushujaa: “Hamjui kitu ninyi, inapasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, kuliko taifa lote kupotea.” Hata kama Yesu ni mtakatifu hivyo, lazima aondoke njiani. Alikuwa, akihafifisha mamlaka ya wazee, ikiwa watu wakipoteza imani yao kwa waongozi wao, uwezo wa taifa utaharibika. Baada ya mwujiza huo wafuasi wa Kristo walifanana kama wenye kutaka kupindua nchi. Warumi wangekuja na kufunga hekalu letu na kutuharibu kama taifa. Hivyo ndivyo alivyosema. Maisha, ya mtu huyu wa Galilaya, yana faida gani ukilinganisha na taifa zima? Je, kumwondolea mbali mtu huyu sio kufanya kazi ya Mungu? Ni afadhali mtu mmoja afe kuliko taifa zima kuangamia.TVV 303.4

  Kanuni ya Kayafa aliyofuata ilikuwa ni kanuni ya mataifa aliyoiga. Kanuni hiyo kwamba, mtu mmoja afie taifa, ndiyo iliyofuatwa ikiwafanya kutoa sadaka ya mtu. Kwa hiyo Kayafa akaazimia kumwua Yesu ili kuliokoa taifa lenye hatia, sio kutoka dhambini, ila kuendelea katika dhambi.TVV 304.1

  Katika baraza hili maadui wa Kristo walimthibitishia Kristo kuwa ana hatia kabisa. Roho Mtakatifu alikuwa amewachoma mioyo sana, lakini Shetani aliwavuta waone aibu waliyotiwa na Kristo. Jinsi alivyowadharau na kuwaona kuwa hawana dini. Akidharau ibada zao na kawaida zao za dini. Amewaambia wenye dhambi kuwa wamwendee Mungu moja kwa moja bila kupitia kwa wazee, kwa maana yeye ni Baba mwenye fadhili nyingi. Amedharau Shule ya Manabii, na kudharau huduma za Makuhani, kwa njia hii ametuvunjia heshima kabisa. Hivyo ndivyo walivyosema, kwa hiyo walimwona kuwa mwenye hatia kabisa.TVV 304.2

  Baraza la Sanhedrini lilikubaliana na shauri la Kayafa, kana kwamba ni neno la Mungu isipokuwa watu wachache sana, ambao hawakutoa maoni yao. Wasiwasi ukaisha na kutokubaliana kukamalizika. Wakaazimu kumwua Kristo, wakati utakapopatikana. Makuhani hawa na wakuu, wameingia katika mikono ya Shetani kamili walakini wao waliona kuwa wametenda tendo bora la kupendeza sana. Walijidhania kuwa wanatafutia taifa lao fanaka na baraka na wokovu.TVV 304.3

  Watu wasipotafakari sana juu ya Yesu, wataangukia kwao wao kwa wao, baraza lilichelewesha matimizo ya kile walichoamua. Mwokozi alijua kuwa mazimio yao yatatimizwa karibuni, lakini haikumpasa kujiweka katika shida pasipo sababu kwa hiyo aliondoka katika wilaya hiyo, pamoja na wanafunzi wake.TVV 304.4

  Yesu sasa alikuwa amefanya kazi muda wa miaka mitatu kamili, ulimwenguni. Hali yake ya kujikana nafsi, na ukarimu na upendo ilijulikana kwa wote.TVV 304.5

  Walakini muda mdogo huo, ulikuwa mrefu mno kwa walimu. Mwenye huruma zote za kila namna kwa wanadamu, alifukuzwa, kama asiyefaa watu. Aliyevunja nguvu za kaburi na kuwatoa waliokuwamo humo, aliyetoa mafundisho ya kutoa watu usingizini, alishindwa kufikia mioyo ya wale wenye chuki waliofishwa, na walioendelea kwa ukaidi kukataa nuru.TVV 304.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents