Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini la Vizazi Vyote

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Yesu Alitamani Huruma za Kibinadamu

    Roho ya binadamu hutamani sana kupata huruma wakati wa mateso. Kristo alishikwa na kiu hii hadi katika kina ya Umbile lake. Aliwajia wanafunzi wake akitamani kusikia maneno yenye faraja. Alitamani kujua kuwa wanamwombea yeye na kujiombea pia. Uovu wa dhambi ulionekana kuwa giza kiasi gani!. Jaribu la kutaka kuwaachia wanadamu wabebe hatia yao wenyewe, wakati Mwenyewe akiwa hana hatia mbele za Mungu lilitisha nmo. Ikiwa tu angelijua kuwa wanafunzi wake wanamwunga mkono, angepata nguvu na kufarijika.TVV 388.1

    Lakini “akawakuta wamelala usingizi.” Kama angaliwakuta wakitafuta maficho kwa Mungu, ili nguvu za Shetani zisiweze kuwashinda, angalifarijika. Lakini lile onyo la “Kesheni, na kuomba.” Hawakuwa wamejali wakukusudia kumkana Bwana wao, lakini ilionekana kuwa wamepigwa na fadhaa ambayo wangeishinda kama wangeendelea kumsihi Mungu kwa maombi. Wakati Mwokozi alipohitaji mno maombi yao, walilala usingizi.TVV 388.2

    Wanafunzi waliamshwa na sauti ya Yesu, lakini hata kidogo hawakumtambua, uso wake ulikuwa umebadilika kwa huzuni. Yesu alimwambia Petro, Je “Simoni, umelala? Hukuweza kukesha saa moja? Kesheni muombe, msije rnkaingia majaribuni; roho i radhi ila mwili ni dhaifu.” Yesu aliogopa kuwa katika hali hiyo waliyo nayo hawataweza kustahimili kusalitiwa kwake na kifo chake.TVV 388.3

    Mara tena Mwana wa Mungu akashikwa na uchungu usiokuwa wa kibinadamu, akizimia’ na kutaabika alijikokota kurudi mahali pa pambano lake la awali. Maumivu yake yalikuwa makali kuliko mwanzo. “hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka chini.” Miti ya mitende na mingine ilikuwa ndiyomashahidi wa uchungu wake. Kutoka katika majani ya matawi yake yalidondoka matone mazito ya umande, juu ya mwili wake uliodhoofika kana kwamba viumbe vya asili vilimlilia Mwumbaji wao akipambana mwenyewe dhidi ya nguvu za giza.TVV 388.4

    Muda si kitambo, Yesu alikuwa amesimama imara kama mwerezi, kukabiliana na dhoruba ya upinzani uliokuwa umemalizia hasira yake kwake. Sasa alifanana na mwanzi mwororo ulipigwa na kukunjwa na dhoruba yenye hasira. Kama aliyetukuzwa tayari, alikuwa amedai umoja na Mungu. Sasa sauti yake ikasikika katika upepo uliotulia wa jioni ikiwa imejaa uchungu wa kibinadamu:TVV 388.5

    “Baba yangu, ikiwa haiwezekani kikombe hiki kiniepuke nisipokunywa, mapenzi yako yatimizwe.”TVV 388.6

    Kwa mara nyingine tena Yesu alitamani maneno ya faraja kutoka kwa wanafunzi wake ambayo yangemwondolea kivuli cha giza lililotanda karibu litamshinda. Lakini macho yao yalikuwa mazito kwa usingizi, “wala hawakujua la kumjibu.” Waliuona uso wake umejaa jasho la damu, kutokana na mahangaiko makuu, lakini uchungu wa mahangaiko ya mawazo wanafunzi wake hawakuweza kuelewa. “(Uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu).” (Isaya 52:14).TVV 389.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents